Chipsi za viazi vitamu

Maandalizi; dakika 15
Muda wa kupika; dakika 15
Muda jumla; dakika 30

Mahitaji

500g/ nusu kilo viazi citamu
Vijiko 4 vya chakula cornstarch
Vijiko 4 vya chakula maji ya baridi
Mafuta ya kukaangia
Chumvi kwa kuonja

Maelekezo

Menya na katakata viazi kama chipsi

Osha na kukausha viazi kwa kutumia tissues za jikoni. Ukitumia kitambaa kinaweza kubadilika rangi, kuwa muangalifu

Changanya cornstarch na maji kwenye bakuli, ongeza viazi uchanganye vizuri

Kwenye kikaango, moto mkali kiasi, chemsha mafuta hadi yachemke. Weka viazi,  usijaze sana kikaangio, acha viive kwa nafasi na hakikisha havishikani

Kaanga mpaka vikaribie kuiva, visipate rangi ya kahawia bado. Toa kwenye mafuta, kausha mafuta kwa kutumia gazeti, mfuko wa karatasi au tissue za jikoni

Ukimaliza kukaanga na kufuta mafuta vyote, zirudishe tena kwenye mafuta kukaanga kwa mara ya pili kwa dakika 1 hadi 2, au mpaka ziwe na rangi ya kahawia na zikauke vizuri

Pakua mafuta yachuje kwenye tissues au chujio la bati, nyunyizia chumvi au viungo vyovyote utakavyopenda

Enjoy

10 Replies to “Chipsi za viazi vitamu”

Leave a Reply