Chapati za shawarma

Maandalizi; dakika 10
Muda wa kupika; dakika 10
Muda jumla; dakika 20
Inatengeneza chapati 4 za wastani

Mahitaji

Kikombe 1 unga wa ngano + 2 vijiko 2 vya chakula wa kusukumia
¼ kijiko cha chai chumvi
Vijiko 2 vya chakula siagi
1/3 (theluthi) kikombe + vijiko 2 vya chakula maziwa
Kijiko 1 cha chai kitunguu saumu
Siagi ya kukaangia

Maelekezo

Kwenye bakuli la wastani linaloweza tumika kwenye microwave, changanya vijiko 2 vya chakula siagi na maziwa. Chemsha mpaka siagi iyeyuke, maziwa yatakuwa ya uvuguvugu. (Usipotumia microwave, weka kwenye sufuria ndogo, chemsha dakika 1 hadi 2 mpaka siagi iyeyuke)

Changanya unga wa ngano, chumvi na mchanganyiko wa siagi na maziwa. Kanda mpaka unga ulainike vizuri. Paka mafuta bakuli jingine pembeni. Weka unga ndani ya baluli, geuza upande wa juu chini ili pande zote zipate mafuta

Funika bakuli kwa kitambaa kisafi au nailoni za kufunikia chakula, acha unga upoe kwa dakika kama 30

Kanda unga tena, gawanya kwenye madonge madogomadogo manne yaliyolingana

Weka madonge ya unga kwenye sehemu iliyonyunyiziwa unga, funika acha yapumzike kwa dakika chache

Wakati unga unapoa, twanga kitunguu saumu

Changanya siagi iliyolainika na kitunguu saumu kilichotwangwa, weka pembeni

Sukuma kila donge ukubwa wa chapatti, itakuwa nyepesi kiasi kulinganisha na chapati

Kwenye kikaangio kilichochemka katika moto wa wastani, weka chapati. Acha ipike mpaka upande wa chini uwe na rangi ya kahawia kiasi na chapati ianze kutuna kiasi kwa juu

Geuza kwa upande mwingine. Geuza tena pande zote mbili hadi chapati ziive vizuri, ziwe na rangi ya kahawia ila zisikauke. Paka mchanganyiko wa siagi na kitunguu saumu juu ya chapati upande wa juu

Pakua chapatti uweke kwenye sahani iliyofunikwa na kitambaa kisafi: hii inasaidia kulainisha chapati

Endelea na unga uliobakia

Pakua kama utakavyopenda

Enjoy

One Reply to “Chapati za shawarma”

Leave a Reply