Butter Chicken

Maandalizi; dakika 20
Muda wa kumarinate; Masaa 4 hadi 24
Muda wa kupika; dakika 20
Muda jumla; dakika 40 + muda wa kumarinate

Mahitaji

Kwa kuku na kumarinate

500g/  ½ kg minofu ya kuku
¼ kikombe mtindi
½ limao
Kijiko 1 cha chai kitunguu saumu
Kijiko 1 cha chai tangawizi
Kijiko 1 cha chai tandoori masala
Kijiko 1½ cha chai beef bouillon powder
Chumvi na pilipili manga kwa kuonja

Kwa sauce

Kijiko 1 cha chakula mafuta ya kupikia
Vijiko 2 vya chakula siagi
Kitunguu kimoja ukubwa wa wastani
Nyanya 2 kubwa
Kijiko 1 cha chai kitunguu saumu
Kijiko 1 cha chai tangawizi
½ kijiko cha chai coriander powder
½ kijiko cha chai binzari ya pilau
Kijiko 1 cha chai curry powder
Kijiko 1 cha chai chicken bouillon powder
½ kikombe  nyanya ya kopo
¾ kikombe whipped cream
½  kikombe tui la nazi
Majani ya giligilani
½  kijiko cha chai smoked paprika
Pilipili kichaa 2
Chumvi na pilipili manga kwa kuonja

Maelekezo kwa video

Maelekezo kwa picha

Maandalizi ya nyama

Osha, kausha na kukatakata nyama vipande vidogovidogo; twanga tangawizi na kitunguu saumu; kamua maji limao

Kwenye bakuli kubwa, changanya vizuri minofu ya kuku na viungo vyote vya marinade

Funika bakuli vizuri, acha ikae kwenye jokofu kwa masaa 4 hadi usiku kucha ( Ikikaa muda mrefu inapendeza zaidi)

Matayarisho ya sosi

Andaa viungo; katakata pilipili; twanga kitunguu saumu na tangawizi; katakata majani ya giligilani

Weka nyanya na kitunguu kwenye mashine ya kusagia, usage upate rojo

Kwenye kikaango kwatika moto wa wastani, chemsha kijiko 1 cha chakula mafuta. Ongeza nyama, hakikisha haibebani (kama kikaango ni kidogo pika mara mbili). PIka nyama mpaka ikaribie kuiva, isiive kabisa

Hamisha nyama kwenye sahani. Rudisha kikaango kwenye moto, ongeza siagi, ikichemka weka kitunguu saumu, tangawizi na pilipili kichaa

Ongeza rojo ya nyanya na kitunguu uliyoisaga, nyanya ya kopo pamoja na viungo vikavu vyote vya sosi

Funika, acha ipike mpaka nyanya ziive vizuri

Mchanganyiko wa nyanya ukiiva, ongeza tui la nazi na whipped cream

Weka vipande vya kuku kwenye sosi

Funika acha iive kwa moto wa chini kwa dakika kama 5; au mpaka iive vizuri

Ikiiva ongeza majani ya giligilani na kupakua

Tenga kama utakavyopenda

Enjoy

One Reply to “Butter Chicken”

Leave a Reply