Mishikaki ya minofu ya samaki

Maandalizi; dakika 20
Muda wa kumarinate; dakika 15
Muda wa kupika; dakika 10
Muda jumla; dakika 45 

Mahitaji

Samaki na viungo

300g minofu minono ya samaki bila mifupa wala ngozi
¼ kikombe majani ya giligilani
Pilipili kichaa 1
½ kijiko cha chai pilipili ya kukausha
Kijiko 1 cha chakula maji ya limao
Kijiko 1 cha chai tangawizi
Kijiko 1 cha chai kitunguu saumu
Vijiko 3 vya chakula mafuta ya mzaituni (olive oil)
Chumvi na pilipili manga kwa kuonja

Kwa mishikaki

Vijiko 2 vya chakula mafuta ya mzaituni (olive oil)
Hoho nusu x3 (nyekundu, kijani na njano)
Kitunguu maji 1 kikubwa
½ kijiko cha chai cayenne pepper
Chumvi na pilipili manga kwa kuonja ste
Majani ya giligilani na limao ya kutengea

Maelekezo

Loweka vijiti vya mishikaki dakika 15 kabla hujatumia

Osha, kausha na kukatakata samaki vipande usawa wa mishikaki. Nyunyizia chumvi na pilipili manga

Kamua limao; twanga tangawizi na kitunguu saumu

Weka vijiko 3 vya chakula mafuta, tangawizi, kitunguu saumu, pilipili kichaa, pilipili ya kukausha, maji ya limao na majani ya giligilani kwenye mashine ya kusagia chakula kutengeneza rojo

Changanya samaki na rojo ya viungo kwenye bakuli, samaki ashike vizuri viungo

Funika bakuli kwa dakika kama 10 hadi 15 (isikae sana samaki akachambuka)

Katakata hoho na kitunguu maji vipande usawa wa samaki

Changanya hoho, kituunguu, kijiko 1 cha chakula mafuta, cayenne pepper, chumvi na pilipili manga

Chomeka samaki na mchanganyiko wa hoho na kitunguu kwenye vijiti vya mishikaki

Kwenye kikaangio katika moto wa juu kiasi, chemsha kijiko 1 cha chakula mafuta yaliyobakia. Ongeza mishikaki kwenye kikaangio

Pika kila upande mpaka ichanganyike vizuri

Tenga kama utakavyopenda na limao. Pamba na majani ya giligilani

Enjoy

Leave a Reply