Chapati za maziwa na siagi

Maandalizi; dakika 15
Muda wa kusubiri; dakika 40
Muda wa kupika; dakika 15
Muda jumla; lisaa 1 dakika 10

Mahitaji

Vikombe 2 unga wa ngano + vijiko 2 vya chakula wa kusukumia
¾ kijiko cha chai chumvi
Vijiko 3½ vya chakula siagi
¾ kikombe maziwa
Siagi ya kukunjia na kukaangia

Maelekezo

Kwenye bakuli la wastani linaloweza tumika kwenye microwave, changanya vijiko 2 vya chakula siagi na maziwa. Chemsha mpaka siagi iyeyuke, maziwa yatakuwa ya uvuguvugu. (Usipotumia microwave, weka kwenye sufuria ndogo, chemsha dakika 1 hadi 2 mpaka siagi iyeyuke)

Changanya unga wa ngano, chumvi na mchanganyiko wa siagi na maziwa. Kanda mpaka unga ulainike vizuri

Funika bakuli kwa kitambaa kisafi au nailoni za kufunikia chakula, acha unga upoe kwa dakika kama 30

Kanda unga tena, ugawanye kweye madonge 4 yaliyolingana

Weka madonge ya unga kwenye sehemu iliyonyunyiziwa unga, funika acha yapumzike kwa dakika chache

Sukuma kila donge hadi liwe jembamba kama chapati, au zaidi

Paka upande wa juu siagi kiasi iliyoyeyushwa

Kwa kutumia kisu kikali, katakata unga vipande vyembamba sana kwa urefu. Ukikata vyembamba zaidi chapati inachambuka zaidi

Kusanya vipande vyote pamoja kwa ajili ya kukunja

Shikilia pande mbili za mwisho

Vuta taratibu kufanya uwe mrefu zaidi kiasi uanze kukunja. Kunja hadi mwisho utengeneze umbo kama la koni

Dumbukiza ncha ya mwisho katikati kwa ndani ili isifunguke

Rudia hadi umalize zote. Acha tena kwa dakika chache unga upumue

Nyunyizia unga usukume unga hadi zifikie ukubwa wa chapati

Kwenye kikaangio kilichochemka katika moto wa wastani, weka chapati. Acha ipike mpaka upande wa chini uwe na rangi ya kahawia kiasi na chapati ianze kutuna kiasi kwa juu

Geuza kwa upande mwingine. Paka siagi juu ya chapati upande uliopikwa. Geuza tena upande mwingine, paka tena siagi. Geuza tena pande zote mbili hadi chapati ziive vizuri, ziwe na rangi ya kahawia ila zisikauke

Pakua kama utakavyopenda. Enjoy

14 Replies to “Chapati za maziwa na siagi”

Leave a Reply