Tambi za nyama ya kusaga na uyoga

Maandalizi; dakika 10
Muda wa kupika; dakika 30
Muda kwa jumla; dakika 40

Mahitaji

500 g/ nusu kilo nyama ya kusaga
250g/ nusu paketi ya tambi
Kitunguu maji kimoja kikubwa
Nyanya 3 za wastani
Kijiko 1 cha chakula kitunguu saumu cha kusaga
Kijiko 1  cha chakula tangawizi ya kusaga
Nusu x3 hoho mchanganyiko zilizokatwakatwa
Vijiko 3 vya chakula mafuta ya kupikia
Kijiko 1 cha chakula beef bouillon powder
Vikombe 2 uyoga (ukipenda)
Karoti 1 kubwa
Vikopo viwili vya nyanya za kusaga (2 x 70 g)
Chumvi na pilipili manga kwa kuonja
Jibini ya chaguo lako ya kunyunyizia juu (ukipenda)
Majani ya kotimiri ya kunyunyizia kwa juu (ukipenda)

Maelekezo kwa video

Maelekezo kwa picha

Andaa viungo; katakata uyoga, karoti, pilipili hoho na kitunguu maji; twanga kitunguu saumu na tangawizi, weka pembeni

Saga nyanya kwenye mashine ya kusagia kupata rojo, weka pembeni

Kwenye sufuria katika moto wa wastani, chemsha mafuta. Ongeza kitunguu maji. Pika mpaka kilainike ila kisikauke

Ongeza kitunguu saumu na tangawizi. Pika kwa dakika kama 2; au mpaka harufu ya ubichi iishe

Ongeza nyama, chumvi na pilipili manga. Kaanga kiasi mpaka nyama ianze kupata rangi ya kahawia, kama dakika 5

Ongeza rojo ya nyanya na beef bouillon powder. Koroga vizuri, funika na mfuniko. Acha nyama iive moto wa chini kwa dakika kama 15, au mpaka iive vizuri na maji yakaukie. Ikibidi ongeza maji kiasi

Ongeza uyoga na karoti kwa dakika kama 1 nyingine

Weka hoho, acha ziive kwa dakika 1 nyingine

Ongeza nyanya ya kopo na maji kiasi, pika kwa dakika chache; au mpaka mbogamboga ziive kama utakavyopenda. Ipua, weka pembeni

Chemsha spaghetti/ tambi kulinganya na maelekezo ya kwenye pakiti. Zikiiva, zichuje maji halafu zipake mafuta uchanganye vizuri ili zisishikane

Rudisha nyama kwenye moto. Ongeza Tambi kwenye mchanganyiko wa nyama na maji kidogo yakihitajika. Changanya vizuri

Pakua na jibini na majani ya kotimiri kama utapenda

Enjoy

8 Replies to “Tambi za nyama ya kusaga na uyoga”

Leave a Reply