Mkate wa mayai wenye sosi ya ndizi na mdalasini

Maandalizi; dakika 10
Muda wa kupika; dakika 20
Muda jumla; dakika 30

Mahitaji

Mkate wa mayai

Mayai 2
½ kikombe maziwa
½ kijiko cha chai vanilla extract
¼ kijiko cha chai chumvi
½ kijiko cha chai mdalasini
¼ kijiko cha chai kungumanga (nutmeg)
Slesi 4 kubwa za mkate (au 6 ndogo)
Siagi na mafuta kwa ajili ya kukaangia

Sosi ya ndizi na mdalasini

Vijiko 4 vya chakula siagi
¼ kikombe sukari ya brown
Ndizi mbivu 2
¼ kijiko cha chai mdalasini

Maelekezo kwa video

Maelekezo kwa picha

Hatua ya 1; kutengeneza mkate wa mayai

Washa oven joto la 120 degrees C. Kwenye bakuli kubwa changanya vizuri maziwa, mayai, vanilla, chumvi, kungumanga na mdalasini (Kama hutatumia oven ni sawa pia, oveni inasaidia mkate usipoe)

Chovya mkate kwenye mchanganyiko wa mayai; moja moja mpaka zilowane vizuri

Paka kikaango siagi na mafuta ya kupikia ya kutosha. Weka mkate kwenye kikaango

Pika pande zote mbili mpaka mkate uwe na rangi ya kahawia

Weka kwenye oven iliyopata joto ili zisipoe

Hatua ya 2; kutengeneza sosi ya ndizi na mdalasini

Katakata ndizi vipande vya mduara

Kwenye sufuria ndogo katika moto wa wastani yeyusha siagi. Ongeua sukari, koroga mpaka iyeyuke vizuri

Ongeza vipande vya ndizi, changanya vizuri vikolee sosi na vipate joto. Nyunyizia mdalasini, changanya vizuri

Ongeza sosi juu ya mkate. Tenga ya moto

Enjoy

4 Replies to “Mkate wa mayai wenye sosi ya ndizi na mdalasini”

Leave a Reply