Tandoori chicken

Maandalizi; dakika 15
Muda wa kumarinate; masaa 4 hadi usiku kucha
Muda wa kupika; dakika 10
Muda jumla; dakika 25 + muda wa kumarinate

Mahitaji

Kilo 1 mapaja ya kuku
Vijiko 2 vya chakula mafuta ya kupikia/ olive oil
½ kikombe mtindi
Kijiko 1 cha chai tandoori masala
½ limao
Kijiko 1 cha chai kitunguu saumu
Kijiko 1 cha  chai tangawizi
Kijiko 1 cha chai rangi nyekundu ya chakula (ukipenda)
Chumvi na pilipili manga ya kuonja

Maelekezo

Osha na kutoa ngozi mapaja ya kuku kisha uyakaushe majimaji na uchanje chanje nyama. Paka chumvi na pilipili manga kwa kukadiria; Twanga kitunguu saumu na tangawizi; Kamua maji limao

Weka kuku na viungo vyote kwenye mfuko wa kuhifadhia chakula au bakuli kubwa, changanya vizuri kuku ashike viungo. Funga mfuko au endapo utatumia bakuli, funika bakuli vizuri. Hifadhi kwenye jokofu viungo vikolee kwa muda wa masaa 4 au usiku kucha

Choma kuku kwa dakika kama 8 mpaka 10; au mpaka aive vizuri. Unaweza pia kuoka kwenye oven katika moto mkali kwa dakika 15 mpaka 20

Pakua kama utakavyopenda

Enjoy

7 Replies to “Tandoori chicken”

Leave a Reply