Rosti ya Kamba wa nazi na karanga

Muda wa maandalizi; dakika 15
Muda wa kumarinate; dakika 10
Muda wa kupika; dakika 15
Muda jumla; dakika 40

Mahitaji

Kamba na viungo vyake

500g/ nusu kilo Kamba
Vijiko 4 vya chakula mafuta ya kupikia (olive oil)
Kijiko 1 cha chai kitunguu saumu
¼ kijiko cha chai chumvi
¼ kijiko cha chai pilipili ya kukausha

Mbogamboga na rosti

Kitunguu maji 1 cha wastani
Pilipili hoho nusu 3x (nyekundu, kijani na njano)
Vijiko 2 vya chakula majani ya kotimiri
Kitunguu cha majani 1
Pilipili kichaa 2 (ukipenda)
Kikombe 1 tui la nazi
Vijiko 4-6 sosi ya samaki (fish sauce)
Vijiko 2 vya chakula karanga za kusaga
Vijiko 2 vya chakula maji ya ndimu
Kijiko 1 cha chakula sukari ya brown
Vijiko 2 vya chakula tangawizi ya unga

Maelekezo

Kwenye bakuli kubwa, changanya Kamba, kijiko 1 cha chakula mafuta, kitunguu saumu, pilipili ya kukausha na chumvi. Changanya vizuri, acha viungo vikolee kwa dakika kama 10

Kwenye bakuli nyingine ya wastani, changanya tui la nazi, sosi ya samaki (fish sauce), tangawizi, sukari, karanga za kusaga na maji ya ndimu. Changanya vizuri, weka pembeni

Kwenye kikaaangio katika moto mkali kiasi, chemsha kijiko 1 cha chakula cha mafuta (endapo kukaangio chako ni kidogo, weka nusu nusu) Ongeza Kamba, pika mpaka waive ila wasikauke, kama dakika 2 kila upande

Wakiiva hamishia kwenye sahani, weka pembeni

Ongeza kijiko 1 cha mafuta kwenye kikaangio. Ongeza kitunguu maji na pilipili hoho. Pika mpaka viive kama utakavyopenda wewe

Ongeza mchanganyiko wa nazi na karanga. Changanya vizuri, ikichemka punguza moto iive moto wa chini kwa dakika kama 5. Ongeza maji kiasi yakihitajika

Ongeza majani ya kitunguu, pilipili kichaa na majani ya kotimiri, changanya vizuri

Ongeza kamba, changanya vizuri

Tenga ya moto

3 Replies to “Rosti ya Kamba wa nazi na karanga”

Leave a Reply