Chicken Masala

Maandalizi; dakika 15
Muda wa kumarinate; masaa 2
Muda wa kupika; dakika 25
Muda jumla; dakika 40 + muda wa kumarinate

Mahitaji

Kwa kuku na rosti

Kilo 1 kuku (au kuku 1)
Nyanya 2 kubwa
Vitunguu 2 vya wastani (au 1 kikubwa)
Kijiko 1 cha chakula tangawizi
Kijiko 1 cha chakula kitunguu saumu
Limao 1 dogo
Pilipili kichaa 2
½ kikombe maziwa ya mgando
Vijiko 6 vya chakula mafuta ya kupikia
Majani ya kotimiri kiasi
Chumvi kwa kuonja 

Viungo

Majani 2-4 ya bay (Bay leaves; kutegemea na ukubwa)
Anise star 1
Iliki nzima 4
Karafuu punje 5
Vijiti 1-2 vya mdalasini
Kijiko 1 cha chai garam masala
Vijiko 2 vya chai chicken bouillon powder
½ kijiko cha chai coriander
½ kijiko cha chai binzari ya pilau
½ kijiko cha chai pilipili ya kukausha
½ kijiko cha chai binzari ya manjano
Chumvi kwa kuonja ikihitajika

Maelekezo

Osha, kausha na kuchanja kuku

Twanga kitunguu saumu na tangawizi; kamua maji limao na katakata majani ya giligilani

Kwenye bakuli kubwa, weka kuku, maji ya limao, kijiko 1 cha chakula kitunguu saumu, kijiko 1 cha chakula tangawizi, chumvi na vijiko 2 vya chakula mafuta

Changanya vizuri, funika na hifadhi kwenye jokofu kwa masaa si chini ya 2

Kwenye kikaango katika moto wa juu kiasi, chemsha vijiko 3 vya mafuta. Ongeza kuku, kanga kila upande kwa dakika kama 2 hadi 3; au mpaka rangi ya ngozi iwe kahawia kiasi, isikauke sana. Ipua, weka pembeni

Weka nyanya, kitunguu na pikipili kichaa kwenye mashine ya kusagia kutengeneza rojo (kama hupendi pilipili toa mbegu kabla usage)

Kwenye sufuria au kikaangio, chemsha kijiko 1 cha chakula mafuta. Ongeza viungo vizima vizima; anise star, vijiti vya mdalasini, iliki, karafuu na bay leaf. Kaanga kwa sekunde kama 30, kuwa muangalifu visiungue

Ongeza kitunguu saumu na tangawizi, pika kwa dakika 1 nyingine

Ongeza rojo ya nyanya, kitunguu na pilipili pamoja na viungo vilivyobakia; garam masala, chicken bouillon powder, binzari ya pilau, binzari ya manjano, coriander powder na pilipili ya kukausha

Funika vizuri, acha iive moto wa wastani mpaka nyanya ziive vizuri

Ongeza mtindi, pika kwa dakika 1 nyingine kisha ongeza kuku, changanya vizuri ashike sosi

Punguza moto, funika acha kuku aive moto wa chini kwa dakika 15 mpaka 20; au mpaka kuku aive vizuri alainike kabisa. Ikibidi ongeza maji kiasi

Ongeza majani ya kotimiri

Pakua cha moto na wali wa maji, wali wa biryani, chapatti, viazi au chakula chochote utakachopenda

Enjoy

4 Replies to “Chicken Masala”

    1. Mara nyingi maduka ya wahindi viungo kama hivyo havikosi, jaribu kariakoo. Ukikosa kabisa usiweke, itakuwa nzuri bado. Nitafuatilia viungo in future niwaambia vinapatikana wapi

Leave a Reply