Wali wa kukaanga

Maandalizi; dakika 10
Muda wa kupika; dakika 10
Muda jumla; dakika 20

Mahitaji

Kwa wali na mbogamboja

Vikombe 2 wali uliopikwa
Vijiko 2 vya chakula mafuta ya kupikia
Kijiko 1 cha chai kitunguu saumu
Kitunguu maji 1 cha wastani
Karoti 1
Kikombe 1 maharagwe machanga
Kitunguu cha majani

Kwa sosi

Vijiko 2 vya chakula sosi ya soya
Kijiko 1 cha chakula mafuta ya ufuza (Ukipenda)
Kijiko 1 cha chai tangawizi (ukipenda)
Mbegu za ufuta (ukipenda)

Maelekezo

Andaa viungo; katakata maharagwe, karoti, majani ya kitunguu na kitunguu maji vipande vidogovidogo sana; Twanga kitunguu saumu na tangawizi, weka pembeni

Kwenye kikaangio kikubwa katika moto wa juu kiasi, chemsha mafuta. Ongeza kitunguu saumu mpaka kiive, halafu uongeze kitunguu maji. Pika mpaka kiive

Ongeza karoti na maharagwe machanga. Pika mpaka viive kama utakavyopenda wewe

Ongeza wali changanya vizuri

Changanya sosi ya soya, mafuta ya ufuta na tangawizi kwenye bakuli, weka pembeni. Ongeza mchanganyiko wa sosi na kitunguu cha maji. Pika kwa dakika nyingine 1, ipua

Pakua cha moto

Nyunyizia mbegu za ufuta kwa juu ukipenda

17 Replies to “Wali wa kukaanga”

  1. Dada Jane unatusaidia wengi napenda kubadilisha pishi…ila siunaweza pika zaidi ya vikombe vili vya mchele? Swali lingine mchele tuna chemsha tu ?

    1. Wali pika kiasi unachotaka wewe, zidisha viungo vingine vyote au kadiria kiasi utakachoona kinatosha. Mchele unapika kama wali wa kawaida, mimi nimetumia kiporo cha wali wa kawaida tu wa kuchemsha na maji, mafuta na chumvi. Unaweza pia kuongeza au kupunguza viungo vingine ambavyo unapendelea wewe

  2. Nmejaribu sikujuaga kama naweza tumia soy sauce kwenye wali i was really amazed kilivyoturn out to be waaay delicious, thanks Jane

  3. Dada jane nakupenda utanifanya niwe mwanamke mpambanaji natalajia kua mama ntilie napenda kupika ila sikua najua nitaandaaje chakula viungo kiungo gani nitaweka ilinipate chakula kizur lengo langu naimani litatimia nakupenda dada jane

Leave a Reply