Chapati za kumimina zenye oatmeal na nutella

Maandalizi; dakika 10
Muda wa kusubiri; dakika 30
Muda wa kupika; dakika 20
Muda kwa jumla; dakika 30 na muda wa kusubiri

Mahitaji

Chapati

1/3 kikombe unga wa ngano
1/3 kikombe Oatmeal
Mayai 2
1/4 kijiko cha chai chumvi
Kijiko 1 cha chakula sukari
Kikombe 1 maziwa
Siagi kwa ajili ya kukaangia

Filling

Nutella kiasi chako
Ndizi mbivu 1 iliyokatwakatwa

Maelekezo


Weka oatmeal kwenye mashine ya kusagia chakula, saga ilainike iwe unga

 

Kwenye bakuli kubwa koroga maziwa,  mayai,  chumvi na sukari mpaka ichanganyike vizuri

 

Ongeza unga wa ngano na oatmeal iliyosagwa. Changanya vizuri

 

Funika, hifadhi kwenye jokofu siyo chini ya dakika 30

Kwenye kikaango ambacho hakishiki chini katika moto wa wastani, weka robo kikombe unga. Kwa haraka, sambaza vizuri mchanganyiko wako usambae kikaango kizima. Acha ipike hadi kona zionekane zina rangi ya kahawia kiasi

Kwa kutumia kijiko kipana, geuza chapati upande wa pili, paka siagi upande uliopika

Pika na upande wa chini uive uwe na rangi ya kahawia pia kisha geuza upake siagi. Geuza tena pande zote mpaka iive vizuri

Hamishia chapati kwenye sahani, zipake nutella ongeza na vipande vya ndizi katikati kiasi utakachopenda

Enjoy

 

2 Replies to “Chapati za kumimina zenye oatmeal na nutella”

Leave a Reply