Salad ya kamba, parachichi na embe

Maandalizi; dakika 15
Muda wa kupika; dakika 10
Muda jumla; dakika 25

Mahitaji

Kamba

500g/ nusu kilo kamba
Kijiko 1 cha chai kitunguu saumu
Kijiko 1 cha chai tangawizi
Vijiko 2 vya chakula siagi
Vijiko 2 vya chakula mafuta ya kupikia
Chumvi na pilipili manga kwa kuonja

Salad

Vikombe 4 majani ya salad ya chaguo lako
Kikombe 1 nyanya ndogondogo
Embe 1
Parachichi 1
1/2 kikombe mahindi mabichi
Kitunguu maji 1 kidogo
Majani ya vitunguu ya kuweka juu
Dressing ya chungwa na tangawizi, bonyeza hapa kwa recipe

Maelekezo

Tengeneza dressing, weka pembeni, jinsi ya kutengeneza bonyeza hapa

Katakata kitunguu maji, weka maji ya limao na chumvi, weka pembeni. (unaweza pia kuweka siki, ona recipe hapa)

Twanga tangawizi na kitunguu saumu

Kwenye kikaangio katika moto wa juu kiasi, yeyusha siagi halafu ongeza mafuta. Ikichemka ongeza kitunguu saumu na tangawizi, kaanga kwa sekunde kama 30, ongeza kamba. Nyunyizia chumvi na pilipili manga kwa juu

Acha waive mpaka wawe na rangi ya pink, dakika 1 hadi mbili, kisha geuza upande wa pili

Wakiiva, geuza pande zote kuhakikisha wameiva vizuri, ipua weka pembeni wapoe kiasi

Wakati kamba wanapoa, andaa viungo vya salad. Osha na kukatakata majani ya salad, kausha kwa tissue za jikoni au kitambaa kisafi, weka pembeni

Katakata nyanya nusunusu; katakata embe na parachichi vipande virefu viredu; katakata na majani ya kitunguu vipande vidogovidogo sana

Pangilia viungo vyote kama utakavyopenda kwenye bakuli, nyunyizia dressing kwa juu

Enjoy

 

 

14 Replies to “Salad ya kamba, parachichi na embe”

    1. Unaweza kuviosha na maji na chumvi au kutengeneza pickle, angalia kwenye post za nyuma. Kama ni kidogo tu havina shida

    2. Unaweza ukakamulia ndimu na ukaweka na chumvi kidogo, ukaviacha kwa mda kupunguza makali kabla haujavichanganya kama unataka visikatike katike badala ya kuosha na chumvi

Leave a Reply