Minofu ya kuku ya kukaanga

Maandalizi; dakika 10
Muda wa kupika; dakika 15
Muda jumla; dakika 25

Mahitaji

500g/ nusu kg minofu ya kuku
Vikombe 2 vya chai chenga za mkate (Bread crumbs)
Vijiko 3 vya chakula unga wa ngano
Mayai 2
Kijiko 1 cha chakula tangawizi na kitunguu saumu
Chumvi na pilipili manga kwa kuonja
Mafuta ya kukaangia

Maelekezo

Osha, kausha na katakata minofu ya kuku vipande virefu vyembamba kiasi

Kwenye bakuli kubwa, Changanya vizuri vipande vya kuku tangawizi na kitunguu saumu; chumvi na pilipili manga. Weka pembeni

Chemsha mafuta kwenye kikaangio moto wa juu kiasi. Wakati mafuta yanachemka, piga yai kwenye bakuli

Paka vipande vya kuku unga wa ngano, halafu chovya kwenye yai lililopigwa na mwishoni zungushia kuku wako chenga za mkate. Kwa kutumia mkono, gandamiza chenga kwenye kuku zishike vizuri

Weka kuku kwenye mafuta yaliyochemka, acha aive hadi awe na rangi ya kahawia na mkavu kwa juu. Unaweza kuongeza na kupunguza moto ikibidi

Kuku akiiva, weka kwenye sahani yenye tissues za jikoni kukausha mafuta

Enjoy

 

 

14 Replies to “Minofu ya kuku ya kukaanga”

    1. Unaweza kununua supermarket ulizia breadcrumbs, au unatengeneza mwenyewe nyumbani kwa kukausha mkate uliopikwa tayari kwenye kikaangio, halafu katakata vipande vidogo, saga kwenye food processor.

  1. Dada Jane you r the best..
    Thank you so much..I have been following up your receip..they are simple na vitu vinakua vitamuu..be blessed..

Leave a Reply