Chipsi za ndizi mzuzu

Maandalizi; dakika 5
Muda wa kupika; dakika 10
Muda jumla; dakika 15

Mahitaji

Ndizi mzuzu tatu kubwa
Vijiko 4 vya chakula chenga za mkate
Mafuta ya kutosha ya kukaangia
Chumvi au viungo vingine

Maelekezo

Menya na kukatakata ndizi umbo la chispi kubwa kubwa kiasi; nyunyizia chumvi na pilipili manga uchanganye vizuri

Kwenye kikaangio kikubwa moto wa juu kiasi, weka mafuta ya kupikia acha yachemke vizuri. Wakati mafuta yanachemka, chovya vipande vya ndizi kwenye chenga za mkate hadi zifunikwe vizuri, kandamiza na mkono chenga zishike kwenye ndizi vizuri

Kaanga kwa dakika mbili upande wa kwanza, geuza kwa dakika moja upande wa pili, au mpaka ziive ziwe na rangi ya kahawia

Ipua kutoka kwenye mafuta, ziweke kwenye sahani yenye tissues zichuje mafuta

Enjoy

14 Replies to “Chipsi za ndizi mzuzu”

Leave a Reply to jane Cancel reply