Kachumbari (dip) ya parachihi

Maandalizi; dakika 10
Muda jumla; dakika 10

Mahitaji

Parachichi moja lililoiva vizuri
Nusu/ ½ ya nyanya ndogo
Maji ya nusu ya ndimu
Kijiko 1 cha chai majani ya giligilani
Chumvi na pilipili manga kwa kuonja
Kitunguu maji kidogo

Maelekezo

Katakata kitunguu vipande vidogovidogo sana, kamulia maji ya nusu ya limao, ongeza na chumvi kiasi. Changanya vizuri, acha ikae kwa muda wa kama nusu saa kabla hujatumia

Toa mbegu na kukatakata nyanya vipande vidogo vidogo sana; katakata majani ya giligilani vipande vidogo sana pia; ponda ponda parachichi mpaka lilainike

Changanya viungo vyote kwenye bakuli. Ongeza chumvi na pilipili manga kwa kuonja. Unaweza ongeza maji ya limao kiasi, ukipenda

Enjoy

 

8 Replies to “Kachumbari (dip) ya parachihi”

Leave a Reply