Nachos/ chipsi za nyama ya kusaga na jibini

Maandalizi; dakika 5
Muda wa kupika; dakika 10 hadi 12
Muda jumla; dakika 15 hadi 17

Mahitaji

Kikombe 1 nyama ya kusaga iliyoungwa
Vikombe 4 vya chipsi aina ya tortilla
1/2 ya kikombe mahindi mabichi
Kikombe 1-2 mozarella cheese
Pilipili kichaa (siyo lazima)
Mbegu za mzaituni (Olives), siyo lazima
Pilipili-halapenyo (jalapeño), siyo lazima

Maelekezo

Washa oven joto la 200 degrees C. Weka chipsi kwenye chombo cha kuokea, zisambae vizuri. Mwagia nyama ya kusaga iliyoungwa juu ya chipsi

Ongeza jibini kisha sambaza kwa juu chipsi nyingine

Ongeza nyama tena, halafu usambaze kwa juu mahindi mabichi, matunda ya mzaituni na Pilipili-halapenyo halafu funika na jibini tena kwa juu

Oka kwa dakika 10 hadi 12, au mpaka jibini iyeyuke vizuri

Enjoy

Leave a Reply