Nyama ya kukaanga na mbogamboga

Maandalizi; dakika 10
Muda wa kupika; dakika 10
Muda jumla; dakika 20

Mahitaji

Nyama na mbogamboga

400g steki laini ya nyama
Vijiko 4 vya chakula mafuta ya kupikia
Hoho nusu x3; rangi mchanganyiko
Kitunguu maji 1
Karoti 1 kubwa
1/2 kikombe kitunguu cha majani
Chumvi na pilipili manga kwa kuonja
Pilipili kichaa 2 (ukipenda)
Majani ya giligilani kiasi (ukipenda)
Mbegu za ufuta (ukipenda)

Sosi

Vijiko 3 vya chakula soy sauce
Kijiko 1 cha chai kitunguu saumu
Kijiko 1 cha chai tangawizi
Kijiko 1 cha chakula maji ya ndimu
Kijiko 1 cha chakula sukari

Maelekezo kwa video

Maelekezo

Ondoa mbegu kwenye hoho halafu uzikatekate pamoja na karoti na kitunguu maji vipande vyembamba virefu. Katakata pilipili, majani ya kitunguu na majani ya giligilani

Katakata nyama vipande virefu

Twanga kitunguu saumu na tangawizi; kamua maji ndimu

Katika bakuli dogo, changanya soya sosi, sukari, maji ya ndimu, kitunguu saumu na tangawizi. Weka pembeni.

Kwenye kikaangio katika moto mkali weka vijiko viwili vya mafuta ya kupikia. Yakichemka ongeza nyama. Isambaze kwenye kikaangio isibebabe

Geuza upande wa pili. Ongeza chumvi na pilipili manga. Kaanga nyama mpaka iive kama utakavyopenda

Hamishia nyama kwenye sahani, weka pembeni

Kwenye kikaango hichohicho, punguza moto uwe mkali wastani. Ongeza vijiko viwili vya mafuta halafu uweke kitunguu maji kwa sekunde chache; kisha ongeza karoti. Pika kwa dakika kama 2

Ongeza pilipili hoho, kaanga ziive kama utakavyopenda wewe

Ongeza nyama, majani ya kitunguu na pilipili kichaa, kaanga kwa sekunde chache halafu mimina mchanganyiko wa sosi. Changanya vizuri kwa dakika kama 1

Ongeza majani ya giligilani, changanya; nyunyizia mbegu za ufuta kwa juu endapo utatumia

Enjoy

 

9 Replies to “Nyama ya kukaanga na mbogamboga”

  1. Ndio, ni rib eye steak ndio nimetumia, naipenda kwa sababu siyo kavu ina mafuta mafuta, ila wengi wanatumia steak ya kawaida. Kwa kiswahili nimetafuta jina nimekosa, ila ni minofu ya kwenye mbavu iliyotolewa mfupa

  2. Ivi dada Jane ivi viungo mama mhyobeef bouillon powder,red wine vinegar, na viungi vingine vingi naona kwenye recipe zako naeza nikavinunua wapi?
    mi ndo naanza kuingia kwenye your wensite leo and i would love to try

    1. Supermarkets au maduka ya wamanga unapata. Uzuri vingi unanunua mara moja unakaa navyo muda mrefu sana. Beef au chicken bouillon powder unaweza kutumia beef cubes za maggi badala yake, zote sawa tu

Leave a Reply