Maandazi/ donuts za sour cream

Maandalizi; dakika 15
Muda wa kusubiri; lisaa 1
Muda wa kupika; dakika 25
Muda jumla; dakika 40 + muda wa kusubiri

Ingredients

Kwa maandazi/ donuts

 

Vikombe 2¼ unga wa ngano (kutoa vijiko 4½ vya chakula)
Vijiko 4½ vya chakula corn starch/ corn flour
Kijiko 1½ cha chai baking powder
Kijiko 1 cha chai chumvi
½ kijiko cha chai kungumanga
½ kikombe sukari
Vijiko 2 vya chakula siagi
Viini 2 vya mayai
½ kikombe sour cream
Mafuta ya kukaangia

Kwa icing sugar

Vikombe 3½ icing sugar
Kijiko 1½ cha chai rice syrup (au corn syrup)
¼ kijiko cha chai chumvi
½ kijiko cha chai vanilla extract
1/3 kikombe maji ya moto

Maelekezo

Hatua ya kwanza; kutengeneza maandazi/ donuts

Kwenye bakuli kubwa, weka vikombe 2¼ unga wa ngano; kisha toa vijiko 4½. Hifadhi unga uliotoa pembeni kwa ajili ya kukandia na kusukumia. Kwenye chekecheo kubwa, chekecha unga wa ngano, baking powder, kungumanga, corn starch/ corn flour na chumvi, weka pembeni

Kwenye bakuli kubwa, changanya mayai na siagi mpaka iwe chenge chenga

Ongeza viini vya mayai, changanya mpaka mchanganyiko ulainike uwe mzito

Ongeza  sour cream kidogo kidogo huku ukichanganya na mchanganyiko wa viungo vikavu; hakikisha mwishoni unaweka unga

Kanda vizuri, unga utakuwa unanata kiasi. Chovya mikono kwenye unga kuushikanisha vizuri

Funika bakuli kwa kutumia kitambaa kisafi cha jikoni au cling wrap. Acha unga utulie kwa lisaa 1 ndani ya jokofu/ friji

Weka unga kwenye sehemu iliyonyunyiziwa unga. Sukuma iwe nyembamba, ila siyo kama chapati; usawa wa maandazi. Tumia kifaa cha kukatia donuts, glasi au kisu kukatakata. Chovya kikatio kwenye unga wa ngano kuzuia kunatanata

Chemsha mafuta kwenye kikaangio kikubwa katika moto wa wastani. Weka donuts/ maandazi kwenye mafuta yaliyochemka, usijaze sana, acha nafasi ya kuumuka. Pika mpaka yawe na rangi nzuri ya kahawia; kama dakika 2 kila upande

Ipua kwenye mafuta, weka kwenye chujio kubwa la bati, gazeti au tissue za jikoni mafuta yachuje vizuri

Hatua ya 2; Kutengeneza icing sugar

Kwenye bakuli nyingine, changanya viungo vyote vya icing sugar mpaka ilainike vizuri

Chovya kila andazi/ donut kwenye icing sugar pande zote

Weka kwenye waya wa jikoni (wire rack) juu ya chombo kipana ili icing sugar ikichuruzike imwagike kwenye chombo

Acha zipoe kwa dakika kama 20 kabla ya kuliwa

Enjoy

 

 

Leave a Reply