Rosti ya nyama ya kusaga na maharagwe

Maandalizi; dakika 15
Muda wa kupika; dakika 30
Muda jumla; dakika 45

Mahitaji

250g/ ¼ kilo nyama ya kusaga
250g/ ¼ kilo maharagwe yaliyochemshwa
Vijiko 2 vya chakula mafuta ya kupikia
Kipande cha mdalasini
Bay leaves 3 ndogo
½ kijiko cha chai mbegu za jira
Kijiko 1 cha chai kitunguu saumu
Kijiko 1 cha chai tangawizi
Nyanya 2 kubwa
Kitunguu 1 kikubwa
Kijiko 1 cha chai maji ya limao (ukipenda)
Pilipili kichaa 2 (ukipenda)
½ kijiko cha chai binzari ya manjano
½ kijiko cha chai coriander powder
Vijiko 2 vya chai beef bouillon powder
½ kijiko cha chai binzari ya pilau
Majani ya kotimiri au giligilani
Chumvi kwa kuonja

Maelekezo kwa video

Maelekezo

Weka nyanya, kitunguu maji, pilipili kichaa na maji ya limao kwenye mashine ya kusagia kutengeneza rojo; twanga kitunguu saumu na tangawizi; katakata majani ya kotimiri, weka pembeni

Kwenye sufuria katika moto wa wastani, chemsha mafuta. Ongeza kipande cha mdalasini, bay leaves na mbegu za jira. Kaanga kwa sekunde kama 30, kisha ongeza kitunguu saumu na tangawizi. Pika mpaka vilainike vizuri na harufu ya ubichi iishe; kama dakika 1

Ongeza nyama, pika kwa dakika kama 5, au mpaka rangi nyekundu iishe kabisa

Ongeza rojo ya nyanya na kitunguu. Weka viungo vikavu pia; beef bouillon powder, binzari ya pilau, binzari ya manjano na coriander powder. Ongeza maji kiasi na chumvi kwa kuonja

Funika sufuria, acha nyama iive kwa dakika kama 15; au mpaka nyama iive vizuri kabisa, geuza pale itakapobidi

Ongeza maharagwe yaliyochemshwa na ½ kikombe maji endapo maji yatakuwa yamekauka sana

Koroga vizuri, funika tena. Acha iive vizuri kabisa, kwa dakika kama 10; geuza itakapobidi

Weka majani ya kotimiri, changanya vizuri

Pakua kama utakavyopenda

Enjoy

Leave a Reply