Uji wa mchele na maziwa

Maandalizi; dakika 5
Muda wa kuloweka mchele; dakika 30
Muda wa kupika; dakika 20
Muda jumla; dakika 25 + muda wa kuloweka mchele

Mahitaji

Mchele kikombe 1
Maji vikombe 4
Maziwa vikombe 3-4
Chumvi kwa kuonja
Asali au sukari (ukipenda)
Mdalasini (ukipenda)

Maelekezo

Osha na kuloweka mchele kwa dakika kama 30 au usiku kucha

Kwenye sufuria katika moto mkali kiasi, chemsha maji. Maji yakichemka weka mchele, acha upike kwa dakika kama 3 mpaka 4

Ondoa mchele kwenye maji, chuja maji

Chemsha maziwa. Weka mchele na chumvi kwenye maziwa yanayochemka. Punguza moto uwe moto wa chini.

Pika kwa moto wa chini kwa dakika 10 hadi 15, huku ukigeuza mara kwa mara usishike kwenye sufuria, mpaka maziwa yakauke na wali uive. Unaweza kuongeza maziwa zaidi endapo utataka wali wako ulainike zaidi

Pakua kwenye bakuli, ongeza asali au sukari, nyunyizia na mdalasini kwa juu. Kula ukiwa wamoto, wabaridi au vuguvugu, utakavyopenda wewe

Enjoy!

 

 

 

 

 

 

 

9 Replies to “Uji wa mchele na maziwa”

Leave a Reply