Maandalizi; dakika 10
Muda wa kupika; dakika 15
Muda jumla; dakika 25
Mahitaji
250g/ ¼ kilo tambi chaguo lako
Vijiko 3 vya chakula mafuta ya kupikia
Vijiko 3 vya chakula siagi
Kijiko 1 cha chai kitunguu saumu na tangawizi
Gramu 400 za Kamba wadogo (unaweza kutumia nusu kilo pia)
¾ kikombe mvinyo nyeupe
½ kikombe maji ya limao
Chumvi na pilipili manga kwa kuonja
½ kikombe nyanya ndogondogo
Vijoko 3 vya chakula jibini (cheddar cheese au utakayopenda)
Kijiko 1 cha chakula majani ya chives (vitunguu vya majani)
Maelekezo
Andaa viungo; twanga kitunguu saumu na tangawizi; kwangua jibini; katakata nyanya nusunusu; katakata majani ya chives; kamua maji limao, weka pembeni
Kwenye sufuria kwenye moto wa wastani, chemsha tambi kulingana na maelekezo ya kwenye pakiti. Hakikisha hazilainiki sana. Chuja maji, weka pembeni
Kwenye sufuria au kikaangio katika moto wa wastani, yeyusha siagi; ongeza mafuta ya kupikia. Kaanga kitunguu saumu hadi kilainike na harufu ya ubichi itoke, kama dakika 1. Ongeza kamba, kaanga kwa dakika kama 3 pande zote. Wasiive sana wakakauka
Ongeza mvinyo, maji ya limao na chumvi; Ongeza nyanya, acha ziive kwa dakika 1
Ongeza tambi pikwa, halafu nyunyizia jibini na majani ya kitunguu (chives). Changanya vizuri
Pakua cha moto
Enjoy