Tambi za kukaanga na nyama na brokoli

Maandalizi; dakika 10
Muda wa kupika; dakika 15
Jumla muda; dakika 25

Mahitaji

Kwa sosi

Vijiko 3 vya chakula sosi ya soya
Vijiko 2 vya chakula hoisin sauce
Kijiko 1 cha chakula mafuta ya ufuta
1/2 kijiko cha chai pilipili ya kukausha (ukipenda)

Kwa nyama, tambi na brokoli

300g steki laini ya nyama
250g/ nusu pakiti ya tambi
Vikombe 2 brokoli
Kijiko 1 cha chai tangawizi na kitunguu saumu
Vijiko 2 vya chakula mafuta ya kupikia
Chumvi na pilipili manga kwa kuonja

Maelekezo

Kata nyama vipande vyembamba virefu; katakata brokoli; twanga kitunguu saumu na tangawizi

Kwenye bakuli kubwa, changanya nyama, kitunguu saumu, tangawizi, kijiko 1 mafuta, chumvi na pilipili manga. Changanya vizuri, funika kwa dakika 10 viungo vikolee

Wakati viungo vinakolea kwenye nyama, kwenye sufuria katika moto wa wastani, chemsha tambi kulingana na maelekezo ya kwenye pakiti

Ongeza brocoli dakika 2 au 3 (kulingana na upendeleo wako) kabla ya tambi kuiva

Ipua tambi, chuja maji uzioshe na maji ya baridi kisha zipake mafuta kiasi ili zisigandane, weka pembeni. Kwenye bakuli ndogo changanya sosi ya soya, hoisin sauce, mafuta ya ufuta na pilipili ya kukausha. Changanya vizuri, weka pembeni

Kwenye kikaangio katika moto wa juu kiasi,  kaanga nyama na kijiko 1 cha mafuta kilichobakia, hakikisha imesambaa vizuri kwenye kikaango bila kubebana. Kaanga kwa dakika kama 3 hadi 4, (au iive kama unavyopenda)

Ogeza tambi na brokoli, changanya vizuri zipate moto; kama dakika 1

Ongeza mchanganyiko wa sosi, pika kwa dakika moja nyingine

Pakua za moto

Enjoy

 

 

3 Replies to “Tambi za kukaanga na nyama na brokoli”

Leave a Reply