Sosi ya chimichurri 

Maandalizi; dakika 10
Muda wa kusubiri; dakika 10
Muda jumla; dakika 20

Mahitaji

½ kikombe mafuta ya mzaituni (olive oil)
Vijiko 2 vya chakula siki (red wine vinegar)
½ kikombe majani ya giligilani
¼ kikombe majani ya mnanaa (siyo lazima)
Punje 3-4 za kitunguu saumu
Pilipili kichaa 2
¾ kijiko cha chai oregano
Kijiko 1 cha chakula chumvi
Pilipili manga kwa kuonja

Maelekezo

Katakata pilipili vipande vidogo sana (bila mbegu na shina); Katakata majani ya giligilani na mnanaa vipande vidogo pia; saga au twanga kitunguu saumu (unaweza pia kutumia vegetable chopper)

Weka viungo vyoke kwenye bakuli. Changanya vizuri. Acha mchanganyiko utulie kwa dakika kama 5 hadi 10 ili harufu ya viungo ikolee kwenye mafuta

Tumia kama inavyohitajika

Enjoy

3 Replies to “Sosi ya chimichurri ”

    1. Ndio, unaweza kuhifadhi kwenye friji kwa wiki kama 2, najua wengine wanahifadhi muda mrefu zaidi. Ni nzuri pia ukiblend, unaweza tumia kama chachandu

Leave a Reply