Salad ya kuku, parachichi na sosi ya Chimichurri

Maandalizi; dakika 20
Muda wa kupika; dakika 10
Muda jumla; dakika 30

Mahitaji

Kwa kuku

Sosi ya Chimichurri;  kwa recipe bonyeza hapa
500g/ nusu kilo minofu ya kuku bila ngozi wala mifupa

Kwa salad

Vijiko 2 cha chakula mafuta ya kupikia
Vikombe 4 majani ya salad utakayopenda
Nyanya 1
Kitunguu 1 cha wastani
Parachichi 1
1/2 kikombe mahindi

Maelekezo

Osha kitunguu kwa chumvi, maji ya limao au  siki

Tengeneza sosi ya Chimichurri; kwa maelekezo bonyeza hapa

Weka kuku kwenye bakuli kubwa, ongeza vijiko 4 vya chakula vya sosi ya Chimichurri. Changanya vizuri kuku akolee viungo.  Funika bakuli, weka kwenye jokofu kwa dakika si chini ya 20. Hifadhi sosi ya Chimichurri iliyobakia kwenye jokofu kwa kutumia kwenye saladi ikiwa tayari

Weka kuku kwenye kikaangio chenya mafuta yaliyochemka katika moto wa wastani. Acha aive upande mmoja hadi awe na rangi ya kahawia, asiungue

Geuza upande wa pili, acha apike hadi aive vizuri, angalia asikauke

Ipua kuku, acha apoe kidogo kisha katakata vipande virefu virefu

Wakati kuku anapoa, osha, kausha na kukatakata majani ya salad; katakata nyanya na parachichi, weka pembeni

Pangilia viungo vyote kwenye bakuli kubwa kama utakavyopenda, nyunyizia sosi ya Chimichurri iliyobakia kwa juu

Enjoy

Leave a Reply