Cinnamon rolls

Maandalizi; dakika 10
Muda wa kupika; dakika 20-25
Muda wa kusubiri; masaa 2
Muda jumla; masaa 2 dakika 30

Mahitaji

Maandalizi ya hamira

Kikombe 1 maziwa ya uvuguvugu
¼ kikombe siagi iliyoyeyushwa
Vijiko 5 vya chakula sukari
Vijiko 2½ vya chai hamira

Kwa kukandia unga

Yai 1 lililopigwa
Vikombe 3½ unga wa ngano
¼ kijiko cha chai chumvi
Kijiko 1 cha chai mafuta ya kupikia

Mahitaji ya kukunjia

½ kikombe sukari ya kahawia
Viko 2 vya chakula mdalasini
Vijiko 2 vya chakula siagi iliyoyeyushwa

Icing

½ kikombe cream cheese
Vijiko 2 vya chakula siagi
Vijiko 2 vya chakula maziwa
Kijiko 1 cha chai vanilla extract
Kikombe 1 icing sugar

Maelekezo

Kwenye bakuli kubwa, changanya kikombe 1 maziwa ya uvuguvugu, ¼ kikombe siagi iliyoyeyushwa, vijiko 5 vya chakula sukari na vijiko 2½ hamira. Changanya vizuri, funika bakuli na kitambaa kisafi; acha iumuke kwa dakika kama dakika 10

Ongeza yai lililopigwa na ¼ kijiko cha chai chumvi kwenye mchanganyiko, changanya vizuri kisha uweke unga wa ngano . Kanda mpaka unga ulainike vizuri. Paka unga mafuta kwa juu pande zote

Funika bakuli. Acha unga uumuke kwenye sehemu yenye joto kwa lisaa moja, au mpaka uumuke mara mbili ya ukubwa wake. Kama una muda, unaweza kukanda na kuumua tena mara ya pili

Sukuma unga wote kwa pamoja kwenye sehemu iliyonyunyiziwa unga wa ngano. Sukuma siyo mduara, fanya upande mmoja uwe mrefu kuliko mwingine

Paka vijiko 2 vya chakula vya siagi iliyoyeyushwa kwa juu kisha nyunyizia vizuri kwa juu sukari na mdalasini

Kwa utaratibu, kunja kuanzia upande mmoja mpana. Zungusha hadi mwisho kabisa. Ukifika mwisho bonyeza kiasi ili usifunguke

Katakata vipande 12 hadi 15

Panga kwenye chombo cha kuokea kilichopakwa mafuta kwa chini. Funika chombo na kitambaa kisafi, acha unga uumuke kwa dakika 30 au mpaka ukubwa mara mbili yake

Wakati unga unaumuka, washa oven joto la 175°C | 350°F, au andaa mkaa kwa ajili ya kuoka. Oka cinnamon rolls kwa dakika kati ya 20-25, au mpaka uwe na rangi ya kahawia kwa mbali kiasi. Ipua, acha zipoe kiasi

Wakati cinnamon rolls zinaiva, andaa icing sugar. Changanya cream cheese, siagi na vanilla mpaka ilainike vizuri. Ongeza icing sugar, koroga hadi iwe laini kabisa

Mwagia icing sugar kwa juu

Enjoy zikiwa za moto au hata zikipoa

Enjoy

4 Replies to “Cinnamon rolls”

Leave a Reply