Kuku wa kukaanga na viungo vikavu

Maandalizi; dakika 15
Muda wa kupika; dakika 15
Muda jumla; dakika 30

Mahitaji

Kuku 1 mkubwa
Vijiko 6 vya chakula unga wa ngano
Kijiko 1 cha chakula curry powder
Vijiko 1½ vya chai tangawizi ya unga
Vijiko 2 vya chakula chicken bouillon powder
½ kijiko cha chai pilipili manga
Chumvi kwa kuonja
Mafuta ya kukaangia

Maelekezo

Osha, katakata na kuchanja kuku kisha umpake chumvi

Kwenye sahani pana, weka unga wa ngano, curry powder, chicken bouillon powder, tangawizi ya unga na pilipili manga, changanya vizuri

Paka vipande vya kuku mchanganyiko wa viungo, ishike vizuri kabisa

Kwenye kikaangio katika moto wa wastani (ongeza na kupunguza moto ikibidi) chemsha mafuta. Yakichemka, weka kuku kwenye mafuta, hakikisha hujazi sana kikaangio, acha waive kwa nafasi. Endapo kikaangio ni kidogo, pika kidogokidogo

Kaanga kuku kila upande mpaka awe na rangi ya kahawia au aive vizuri kabisa

Hamishia kwenye wire rack, chujio la bati au karatasi za jikoni ili mafuta yachuje

Pakua kama utakavyopenda

Enjoy

3 Replies to “Kuku wa kukaanga na viungo vikavu”

Leave a Reply