Rosti ya maini ya ngo´mbe

Matayarisho; dakika 15
Muda wa kupika; dakika 20
Muda jumla; dakika 35

Mahitaji

500g/ nusu kilo ya maini
Vijiko 4 vya chakula mafuta ya kupikia
Kijiko 1 cha chai tangawizi
Kijiko 1 cha chai kitunguu saumu
Hoho mchanganyiko nusu x3
Karoti 1
Nyanya 2 za wastani
Kitunguu maji 1 cha wastani
Pilipili kichaa 1
Chumvi kwa kuonja
Majani ya giligilani (ukipenda)

Maelekezo

Weka nyanya na pilipili kwenye mashine ya chakula utengeneze rojo

Menya, osha na katakata maini; katakata kitunguu maji, pilipili hoho na karoti vipande vidogovidogo vya mraba; twanga kitunguu saumu na tangawizi; katakata majani ya giligilani

Kwenye sufuria au kikaango kikubwa katika moto mkali kiasi, weka mafuta. Ongeza kitunguu maji, kitunguu saumu na tangawizi. Kaanga kwa dakika kama 2, au mpaka viive vizuri ila visikauke

Ongeza maini. Weka na chumvi kwa kukadiria. Endelea kukaanga huku ukigeuza geuza hadi maini yapate rangi ya kahawia kiasi, ila yasiive kabisa

Ongeza rojo ya nyanya na pilipili. Funika acha iive kwa moto wa wastani mpaka nyanya ziive vizuri, dakika kama 4

Ongeza karoti kwa dakika kama 1 kisha weka pilipili hoho kwa dakika nyingine 1; au mpaka viive kama utakavyopenda. Unaweza pia kuongeza maji kidogo ukipenda mchuzi

Pakua kama utakavyopenda

Enjoy

9 Replies to “Rosti ya maini ya ngo´mbe”

Leave a Reply