Mkate wa kukaanga wenye mayai na mdalasini

Maandalizi; dakika 10
Muda wa kupika; dakika 20
Muda jumla; dakika 30

Mahitaji

Kijiko 1 cha chakula unga wa ngano
ยฝ kikombe maziwa
ยผ kijiko cha chai chumvi
Mayai 2
ยผ kijiko cha chai mdalasini
ยฝ kijiko cha chai vanilla
Kijiko 1 cha chai sukari nyeupe
Mkate vipande 6
Siagi na mafuta kwa ajili ya kukaangia

Maelekezo

Kwenye bakuli kubwa, weka maziwa, mayai, chumvi na sukari. ongeza maziwa koroga vizuri. Ongeza vanilla, mdalasini naunga wa ngano . Changanya hadi ilainike vizuri

Paka mafuta na siagi kiasi kwenye kikaangio katika moto wa wastani. Loweka mkate kwenye mchanganyiko wa unga na mayai hadi ukolee vizuri. Weka mkate kwenye kwenye kikaango

Pika pande zote mpaka uwe na rangi ya kahawia ila usikauke wala kuungua

Pakua yamoto

Enjoy na maple syrup, matunda, asali, ice cream na kingine chochote utakachopenda

25 Replies to “Mkate wa kukaanga wenye mayai na mdalasini”

  1. Thank you Jane.. am learning alot mydear keep on posting hata siku post 2 za mapishi tofaut jaman… my request hapa tuwekee variieties ya soup lakin za kiswahili jaman isiwe too complicated

  2. Jane wangu tuwekee na jinsi ya kupika maandazi yale malaini loh… na vi bake bake tofaut vya chai tunapata shida jaman ya breakfast majumban…asante kwa msaada huu na elimu kwetu

  3. Da Jane ili kupata hiyo rangi ya njano unachanganya nini au ni mayai ya kienyeji coz nimetumia vt vyote but sijapata dat colour

  4. Ndo kilichofail but there so good na nimeanza biashara tayar thaxxx much sister need to learn more from you

    1. Am happy imekusaidia kwenye biashara, Mungu akutangulie my dear. Vitu vingine vinakuja vinaweza kukufaa pia kwa biashara

Leave a Reply