Kamba wa kukaanga na mbogamboha

Maandalizi; dakika 10
Muda wa kupika; dakika 10
Muda jumla; dakika 20

Mahitaji

Kamba na mbogamboga

1/2 kilo kamba
1/4 kilo njegere changa
Karoti 2 za wastani
Kijiko 1 cha chakula kitunguu saumu na tangawizi
Kijiko 1 cha chakula siagi
Vijiko 2 vya chakula mafuta ya kupikia
Chumvi na pilipili manga kwa kuonja

Sosi

Vijiko 2 vya chakula sosi ya soya
Vijiko 2 vya chakula hoisin sauce
Kijiko 1 cha chakula maji ya limao

Maelekezo

Kata ncha za njegere; katakata karoti vipande virefu usawa wa njegere; twanga kitunguu saumu na tangawizi

Kwenye kikaangio katika moto wa juu kiasi, yeyusha siagi halafu ongeza mafuta. Ikichemka ongeza kamba; sambaza vizuri kwenye kikaangio wasibebane. Acha waive mpaka wawe na rangi ya pink, dakika 1 hadi mbili, kisha geuza upande wa pili kwa dakika 2 nyingine. Ongeza kitunguu saumu, tangawizi chumvi na pilipili manga. Kaanga kwa dakika kama 1

Pakua kwenye sahani, weka pembeni

Ongeza kijiko 1 cha chakula mafuta kwenye kikaango, kisha ongeza njegere na karoti. Kaanga kwa dakika kama 3 mpaka 4, au kama utakavyopenda

Ongeza Hoisin sauce, sosi ya soya na maji ya limao, changanya vizuri

Ongeza kamba waliokaangwa awali, changanya vizuri, ipua waliwe wakiwa wamoto

Enjoy

Leave a Reply