Pancakes

Maandalizi; dakika 10
Muda wa kusubiri; lisaa 1
Muda wa kupika; dakika 30
Muda jumla; Lisaa 1 dakika 40

Mahitaji

Vikombe 2 unga wa ngano
¼ kikombe sukari
Vijiko 4 vya chai baking powder
½ kijiko cha chai chumvi
Vikombe 1⅔ maziwa
¼ kikombe, siagi iliyoyeyushwa
Vijiko 2 vya chai vanilla
Yai 1 kubwa

Maelekezo

Kwenye bakuli kubwa, chekecha unga wa ngano, sukari, baking powder na chumvi. Changanya vizuri

Ongeza maziwa, siagi iliyoyeyushwa, vanilla na yai. Changanya vizuri ukianzia kukoroga katikati viungo vya majimaji mpaka vikavu; mpaka ulainike vizuri kabisa. (Kunaweza kubaki mabonge mabonge kiasi, siyo tatizo).

Funika bakuli, acha unga upumzike kwa lisaa moja au zaidi

Kwenye kikaangio kisichoshika chini, katika moto wa chini, paka kikaangio siagi kiasi. Unaweza pia kutumua round egg/ pancakes rings au vifaa tofauti kupata umbo la mduara

Mwagia ¼ kikombe ya unga kwenye kikaangio. (Kama unga ni mzito sana, ongeza maziwa kiasi kulainisha). Pika mpaka upande wa chini uwe kahawia, na pancake itune kwa juu

Geuza, pika mpaka pande zote ziwe za kahawia 

Rudia kwa unga uliobakia hadi umalize. Tenga na utakachopenda maka matunda, asali, maple syrup, sosi ya chocolate, ice cream or frozen yoghurt; au hata hivihivi bila kitu

Enjoy

 

10 Replies to “Pancakes”

Leave a Reply