Rosti ya nyama ya kondoo

Maandalizi; dakika 15
Muda wa kumarinate; masaa 2
Muda wa kupika; dakika 45
Muda jumla; lisaa 1

Mahitaji

Nyama ya kondoo

Kilo 1 nyama ya mbavu za kondoo
Kijiko 1 cha chakula kitunguu saumu na tangawizi
Vijiko 2 vya chakula mafuta ya kupikia
Chumvi na pilipili manga kwa kuonja

Viungo

Karafuu punje 4
Iliki nzima 4
Majani madago 4 ya bay leaves
Kipande cha mdalasini
Anise star 1
Kijiko 1 cha chai coriander powder
Kijiko 1 cha chai binzari ya pilau
½ kijiko cha chai binzari ya manjano
½ kijiko cha chai cayenne pepper

Sosi

Vijiko 2 vya chakula mafuta ya kupikia
Nyanya 3 za wastani
Kitunguu maji 1 kikubwa
Kijiko 1 cha chai tangawizi na kitunguu saumu
Pilipili kichaa 2
Vikombe 2 maji
Chumvi kwa kuonja
Majani ya kotimiri au giligilani kiasi

Maelekezo

Twanga kitunguu saumu na tangawizi kwa ajili ya nyama

Weka nyama, kitunguu saumu, tangawizi, chumvi na mafuta kwenye bakuli kubwa au mfuko. Changanya vizuri, marinate kwa masaa 2 au usiku kucha

Weka nyanya, kitunguu na pilipili kwenye mashine ya kusagia chakula kutengeneza rojo

Twanga kitunguu saumu na tangawizi kwa ajili ya sosi; katakata na majani ya kotimiri/ giligilani vipande vyembamba, weka pembeni

Kwenye sufuria/ kikaango moto wa juu kiasi, chemsha mafuta kisha ukaange kitunguu saumu na tangawizi kwa dakika moja. Ongeza nyama, weka kwa kusambaza isibebane. Kaanga kila upande mpaka ianze kuwa na rangi ya kahawia

Ongeza viungo vizimavizima; mdalasini, iliki, karafuu, anise star na majani ya bay leaves. Funika, pika kwa dakika kama 2

Ongeza rojo ya nyanya-kitunguu-pilipili kichaa pamoja na viungo vilivyobakia; cayenne pepper, binzari ya pilau, coriander powder na binzari ya manjano. Ongeza chumvi kisha pika imefunikwa mpaka nyanya ziive vizuri

Ongeza maji, funika tena. Acha ichemke moto wa wastani kwa dakika 20 mpaka 30; au mpaka nyama iwe laini kabisa na sosi iwe nzito. Ongeza majani ya giligilani

Pakua ya moto

Enjoy

 

Leave a Reply