Wali wa kukaanga wenye mbogamboga na nanasi

Maandalizi; dakika 10
Muda wa kupika; dakika 15
Muda jumla; dakika 25

Mahitaji

Wali na mbogamboga

Vikombe 2 wali uliopikwa
Vijiko 2 vya chakula mafuta ya kupikia
Kijiko 1 cha chai kitunguu saumu
Kitunguu maji 1 kidogo
Karoti 1 ndogo
1/2 kikombe maharagwe machanga
1/2 kikombe uyoga
1/2 kikombe nanasi lililokatwakatwa
Vitunguu 2 vya majani
Mbegu za ufuta; ukipenda

Sosi

Kijiko 1 cha chakula sosi ya soya (dark) au 2 light
Kijiko 1 cha chakula mafuta ya ufuta
½ kijiko cha chai tangawizi ya unga
¼ kijiko cha chai pilipili manga (nyeupe)

Maelekezo

Kwenye kibakuli kidogo, changanya sosi ya soya, mafuta ya ufuta, tangawizi ya unga na pilipili manga, weka pembeni

Andaa viungo; katakata kitunguu, karoti, maharagwe, uyoga, nanasi na majani ya kitunguu vipande vidogovidogo sana; twanga kitunguu saumu, weka pembeni

Kwenye kikaangio katika moto wa juu kiasi, chemsha mafuta kisha ukaange kitunguu saumu na kitunguu maji hadi vilainike harufu ya ubichi iishe; kama dakika 2

Ongeza karoti na maharagwe machanga. Pika kwa dakika nyingine 2 ukigeuza mara kwa mara. Ongeza uyoga kwa dakika nyingine 2

Weka nanasi, vitunguu vya majani na wali, changanya vizuri

Ongeza mchanganyiko wa sosi. Pika kwa dakika kama 1 ukigeuza mara kwa mara

Pakua cha moto

Enjoy

Leave a Reply