Makange ya kuku wa kuchoma

Maandalizi; dakika 10
Muda wa kupika; dakika 10
Muda jumla; dakika 20

Mahitaji

Kuku 1 wa kuchoma mkubwa
Nyanya 2 za wastani
Vitunguu 2 vya wastani (au 1 kikubwa)
Karoti 1 kubwa
Pilipili hoho nusu x3 (nyekundu, njano na kijani)
Kijiko 1 cha chakula kitunguu saumu na tangawizi
Vijiko 3 vya chakula mafuta
Kijiko 1 cha chakula hoisin sauce (si lazima)
Chumvi kwa kuonja

Maelekezo

Katakata kuku vipande vikubwa vikubwa

Andaa viungo; katakata kitunguu, karoti na pilipili hoho vipande virefu virefu. Katakata nyanya vipande kama 8, au kama unavyopenda, weka pembeni

Kwenye sufuria katika moto wa juu kiasi, chemsha mafuta kisha ukaange kitunguu saumu, karoti na kitunguu maji kwa dakika kama dakika 2

Ongeza nyanya na pilipili hoho. Pika kwa dakika nyingine 2 hadi 3; au mpaka ziive kama utakavyopenda wewe; ukigeuza mara kwa mara

Ongeza kuku na hoisin sauce, changanya vizuri kabisa, ikae kwenye moto kwa dakika kama 1

Pakua ya moto

Leave a Reply