Tambi za kuku, maziwa na jibini

Tambi za kuku, maziwa na jibini
Maandalizi; dakika 5
Muda wa kupika; dakika 20
Muda jumla; dakika 25

Mahitaji

500g/ nusu kilo minofu ya kuku
Vikombe 3 pasta
Vijiko 2 vya chakula mafuta
Kitunguu maji 1
Kijiko 1 cha chai kitunguu saumu
Vikombe 1¼ maziwa fresh
Nyanya 1 kubwa
Kikopo 1 cha nyanya ya kopo (70g)
¼ kijiko cha chai cayenne pepper
Kikombe 1 jibini (cheddar cheese)
Chumvi na pilipili manga kwa kuonja
Majani ya kotimiri kiasi

Maelekezo

Katakata kuku vipande vidogo kiasi; katakata nyanya na kitunguu vipande vidogovidogo; twanga kitunguu saumu; kwangua jibini; katakata majani ya kotimiri vipande vidogo vidogo

Chemsha tambi kutokana na maelekezo ya kwenye pakiti; ipua dakika 2 kabla ziive kabisa

Kwenye sufuria katika moto wa wastani, chemsha mafuta. Ongeza kitunguu maji na kitunguu saumu, kaanga kwa dakika kama 1-2 au mpaka vilainike. Ongeza minofu ya kuku, endelea kukaanga ukigeuza geuza mpaka rangi ya kuku kwa nje isiwe pink tena; ila kuku asiive kabisa kwa ndani. Weka chumvi na pilipili manga

Ongeza nyanya na cayenne pepper, pika kwa dakika nyingine 2-3 au mpaka nyanya zilainike vizuri. Ongeza nyanya ya kopo, changanya vizuri

Ongeza maziwa, changanya vizuri. Acha ichemke kabisa na sosi ianze kuwa nzito kisha uongeze tambi zilizochemshwa awali. Acha ichemke vizuri kwa dakika 2, au mpaka tambi ziive vizuri (ikiwa nzito sana ongeza maziwa kiasi utakachopenda)

Ongeza jibini, changanya vizuri. Ongeza majani ya kotmiri

Pakua ya moto

Leave a Reply