Nyama ya mbavu ya kupika kwenye slow cooker

Maandalizi; dakika 5
Muda wa kupika; masaa 4-8 dakika 8
Muda jumla; masaa 4-8 dakika 13

Mahitaji

1½ kilo nyama ya mbavu (mapande 3)
Kijiko 1 cha chakula chumvi
Kijiko 1 cha chakula pilipili manga
Kijiko 1 cha chakula kitunguu saumu cha unga
Kijiko 1 cha chakula paprika
Kijiko 1 cha chakula oregano
Kijiko 1 cha chakula cayenne pepper
250g/ chupa ndogo ya BBQ sauce

Maelekezo

Paka nyama chumvi, pilipili manga, kitunguu saumu cha unga, paprika, cayenne pepper na oregano. Paka vizuri kwa mkono viungo visambae vizuri kisha paka nusu ya BBQ sauce pande zoze zishike vizuri

Weka nyama kwenye slow cooker kwa kusimamisha

Pika moto wa chini (low heat) masaa 6-8, au moto wa juu (high heat) masaa 3-4 hours; au mpaka zilainike kama utakavyopenda

Hamishia nyama kwenye chombo cha kuokea kwenye oven au grill chenye nyavunyavu ili majimaji yatiririke. Weka chombo kwa chini na aluinium foil kwa ajili ya majimaji yatakayochuruzika. Paka BBQ sauce iliyobakia pande zote za nyama

Oka au choma moto wa juu kwa dakika 5-8 (unaweza pia kutumia mkaa kwa dakika 3-5)

Enjoy

Leave a Reply