Maharagwe ya nazi na binzari ya manjano

Maandalizi; dakika 5
Kupika; dakika 15
Muda jumla; dakika 20

Mahitaji

250g/ robo kilo maharagwe yaliyochemshwa
Vijiko 2 vya chakula mafuta
Kijiko 1 cha chai binzari ya manjano
Kijiko 1 cha chai vegetable seasoning
Kitunguu maji 1 kidogo
Nyanya 1 ya wastani
Kijiko 1 cha chai nyanya ya kopo
Kikombe 1 tui la nazi
Chumvi kwa kuonja

Maelekezo

Weka nyanya na kitunguu kwenye mashine kutengeneza rojo

Chemsha mafuta kwenye sufuria katika moto wa chini kiasi. Ongeza rojo ya nyanya na kitunguu, binzari ya manjano na vegetable seasoning.  Changanya vizuri, funika mpaka iive vizuri

Ongeza maharagwe, tui la nazi na nyanya ya kopo. Funika tena, acha ichemke mpaka sosi iwe nzito. Endapo itakuwa nzito sana, ongeza maji au tui la nazi. Ongeza chumvi zaidi ikihitajika

Enjoy

Leave a Reply