Viazi vya kuponda

Maandalizi; dakika 5
Muda wa kupika; dakika 20
Muda kwa jumla; dakika 25

Mahitaji

500g/ ½ kilo viazi
Lita 1 ya maji
½ kikombe maziwa
Vijiko 2-3 siagi
Chumvi kwa kuonja

Maelekezo

Menya, osha na kukatakata viazi vipande vikubwa vikubwa

Weka viazi kwenye sufuria, ongeza maji ukihakikisha viazi vimefunikwa na maji. Chemsha mpaka maji yachemke, kisha ongeza chumvi. Chemsha mpaka viazi viive vizuri

Viazi vikiiva vizuri ipua, hamishia kwenye chujio kubwa la bati kuchuja maji. Rudisha chujio juu ya sufuria, anza kuponda viazi mpaka vyote vipite kwenye chujio kuhakikisha hakuna mabonge mabonge

Ongeza maziwa na siagi kiasi utakachopenda mpaka upate uzito na radha utakayopenda

Pakua cha moto

Enjoy

2 Replies to “Viazi vya kuponda”

Leave a Reply