Biriyani ya chicken tikka

Maandalizi; dakika 45
Muda wa kumarinate; masaa 4+
Muda wa kupika; lisaa 1 dakika 15
Muda jumla; Masaa 2 + muda wa kumarinate

Mahitaji

Kumarinate nyama

500g/ nusu kilo minofu ya kuku
Kikombe 1 mtindi
Kijiko 1 cha chakula tangawizi na kitunguu saumu
Kijiko 1 cha chakula tandoori masala
Kijiko 1 cha chai cayenne pepper
Kijiko 1 cha chai binzari ya manjano
¼ kikombe mafuta
Kijiko 1 cha chai maji ya limao
Chumvi kwa kuonja

Kwa wali

Vikombe 2 mchele wa basmati
Kijiko cha chai mbegu za jira (cumin seeds)
Bay leaf 1
¾ kijiko cha chai chumvi

Kwa kutengeneza sosi/ gravy

½ kilo viazi ulaya
Kijiko 1 cha chakula tangawizi na kitunguu saumu
Kitunguu maji 1
Nyanya 2 kubwa
Vijiko 4 vya chakula mafuta ya kupikia
Pilipili kichaa 2
1/4 kikombe mtindi

Viungo vya sosi

Kijiko 1 cha chakula garam masala
Kijiko 1 cha chai unga wa giligilani
1/2 kijiko cha chai cayenne pepper
Kijiko 1 cha chai mbegu za jira
Kipande cha mdalasini
Bay leaf 2
Punje 5 karafuu
Punje 5 iliki
Star anise 2

Viungo vya juu/ garnish

Kitunguu maji 1
Zafarani kiasi
¼ kikombe maji ya uvuguvugu
¼ kikombe majani ya giligilani
¼ kikombe majani ya mnanaa
Mafuta ya kukaangia kitunguu

Maelekezo

Hatua ya kwanza; Kumarinate nyama

Osha, kausha na kukatakata minofu ya kuku vipande vya mraba

Changanya viungo vyote vya marinade kwenye bakuli kubwa; mtindi, tangawizi na kitunguu saumu, tandoori masala, cayenne pepper, binzari ya manjano, mafuta, maji ya limao na chumvi kwa kuonja. Ongeza minofu ya kuku, changanya vizuri. Funika viungo vikolee kwa masaa 4 au inapendeza zaidi akikaa  usiku kucha

Hatua ya pili; maandalizi

Ukiwa tayari kupika, andaa mchele kwa kuuosha hadi maji yawe masafi kabisa. Loweka kwenye maji kwa muda wa dakika 30

Ukiloana, chuja maji weka pembeni

Andaa viungo vya sosi/ gravy; menya na kukatakata viazi ukubwa utakaopenda; katakata pilipili vipande vidogovidogo vya mraba; weka nyanya kwenye mashine ya kusagia chakula kutengeneza rojo; katakata na majani ya giligilani na majani ya mnanaa, katakata kitunguu kwa ajili ya sosi na kuweka juu ya biriyani

Loweka zafarani chache kwenye ¼ kikombe cha maji ya uvuguvugu

Hatua ya tatu; Kupika

Washa oven katika joto la 150 degrees C. Kwenye sufuria katika moto wa juu kiasi, chemsha vikombe 4 vya maji. Ongeza mchele, mbegu za jira, bay leaf na chumvi. Pika mpaka wali ukaribie kuiva. Ipua, chuja maji. Weka pembeni

Kwenye kikaangio katika moto wa wastani kaanga kitunguu kwa ajili ya kuweka juu (garnish) mpaka kiwe na rangi ya kahawia ila kisiungue. Hamishia vitunguu kwenye sahani iliyotandazwa tissues za jikoni au chujio la bati ili mafuta yachuje. Weka pembeni kwa ajili ya kuweka juu ya biryani badae

Ukitoa kitunguu, weka viazi kwenye mafuta. Kaanga mpaka vikaribie kuiva, ipua weka pembeni

Kwenye sufuria katika moto wa chini kiasi, chemsha vijiko 4 vya chakula mafuta ya kupikia. Ongeza kitunguu maji, pilipili kichaa na viungo vizimavizima; mdalasini, mbegu za jira, karafuu, star anise na iliki. Kaanga kwa dakika 1-2, kisha ongeza kitunguu saumu na tangawizi upike kwa dakika 3 nyingine

Ongeza rojo ya nyanya na viungo vikavu vilivyoandaliwa kwa ajili ya sosi; giligilani ya unga, cayenne pepper, garam masala na chumvi. Acha ipike mpaka nyanya ziive vizuri

Ongeza nyama na mtindi, koroga vizuri

Funika sufuria, acha nyama iive na  sosi ianze kuwa nzito; ongeza viazi vya kukaanga. Funika tena mpaka sosi ikaribie kukauka kabisa; ibakie kama kikombe 1 cha kuivisha wali

Hatua ya 4; kupangilia biryani

Sambaza nyama na sosi yake chini ya chombo cha kuokea au sufuria nyingine kubwa zaidi. Sambaza wali juu ya nyama

Ongeza na majani ya giligilani, majani ya mnanaa yaliyakatwakatwa kwa ajili ya kuweka juu pamoja na kitunguu cha kukaanga. Nyunyizia kwa juu maji yenye zafarani

Funika na foil, acha wali uive kwenye oven iliyopata moto kwa dakika 15 hadi 20; au mpaka wali uive vizuri. (unaweza pia kupalilia kwa mkaa, au kuoka kwenye oven katika chombo chenye mfuniko). Changanya vizuri. Pakua ya moto

Enjoy

 

Leave a Reply