Red Velvet Cake

Maandalizi; dakika 30
Muda wa kupika; dakika 30-40
Muda wa kusubiri; saa 1 dakika 30
Muda kwa jumla; masaa 2 dakika 30

Mahitaji

Kwa keki

½ kikombe siagi
1½ kikombe sukari nyeupe
Mayai 2
Vijiko 2 vya chakula cocoa powder
¾ kijiko cha chai rangi nyekundu ya chakula gel (vijiko 4 rangi ya maji)
Kijiko 1 cha chai chumvi
Kijiko 1 cha chai vanilla extract
Kikombe 1 buttermilk
Vikombe 2½ unga wa ngano (uliochekechwa)
Kijiko 1½ cha chai baking soda
Kijiko 1 cha chakula siki

Kwa Icing sugar/ frosting

Vijiko 5 vya chakula unga wa ngano
Kikombe 1 maziwa
Kikombe 1 sukari nyeupe
Kikombe 1 siagi (butter)
Kijiko 1 cha chai vanilla extract

Maelekezo

Washa oven joto la 175 degrees C. Paka vyombo 2 vya kuokea (au kimoja kikubwa uje ukate keki vipande 2). Weka siagi na sukari kwenye bakuli kubwa, piga mpaka ilainike vizuri. Ongeza yai moja moja, endelea kupiga mpaka ilainike vizuri kabisa

Kwenye bakuli nyingine, changanya buttermilk, cocoa powder, chumvi, rangi ya chakula na vanilla extract. Changanya ichanganyike vizuri

Ongeza mchanganyiko wa buttermilk na unga wa ngano kidogokidogo kwenye mchanganyiko wa awali (siagi, sukari na mayai), mpaka ichanganyike vizuri kabisa

Kwenye bakuli ndogo au bilauli, changanya siki (vinegar) na baking soda. Ongeza kwenye mchanganyiko wa keki. Changanya vizuri kutumia mkono usitumie mashine, usichanganye sana

Mimina mchanganyiko kwenye chombo/ vyombo vya kuokea. Oka mpaka keki iive vizuri; kama dakika 30-40

Ikiiva, ipua, acha keki ipoe kabisa

Wakati keki inapoa, chemsha maziwa na vijiko 5 vya unga wa ngano katika moto wa chini, ukikoroga mfululizo. Acha uchemke mpaka uwe mzito kabisa. Ipua, acha upoe pembeni

Mchanganyiko ukipoa kabisa; Piga sukari na siagi kwenye bakuli kubwa mpaka ilainike vizuri. Ongeza mchanganyiko wa unga wa ngano na maziwa pamoja na vanilla, endelea kupiga mpaka icing sugar ilainike kabisa

Paka juu ya keki

Katakata kama utakavyopenda

Enjoy

 

 

2 Replies to “Red Velvet Cake”

Leave a Reply to Sarel Cancel reply