Minofu ya kuku ya kukaanga na kitunguu na pilipili hoho (chicken fajitas)

Maandalizi; dakika 5
Muda wa kupika; dakika 15
Muda kwa jumla; dakika 20

Ingredients

250g/ 1/4 kilo minofu ya kuku
Hoho 1/2 mara 3 (nyakundu, kijani na njano)
Kitunguu maji 1
Vijiko 2 mafuta ya kupikia
Kijiko 1 cha chai chicken seasoning
Kijiko 1 cha chai kitunguu saumu na tangawizi
Chumvi na pilipili manga kwa kuonja

Maelekezo

Andaa viungo; katakata kuku, kitunguu na pilipili hoho vipande virefu virefu

Kwenye kikaangio katika moto wa wastani; chemsha mafuta, kisha ongeza nyama ya kuku, chicken seasoning, kitunguu saumu na tangawizi. Kaanga mpaka nyama ikaribie kuiva, ila isiive kabisa

Ongeza kitunguu maji, pilipili hoho, chumvi na pilipili manga

Endelea kukaanga kwa dakika chache, mpaka kuku aive vizuri na mboga mboga ziwe crunchy, zisilainike sana

Pakua, enjoy na chakula utakachopenda

Leave a Reply