Vipapatio vya kuku crispy vyenye sosi ya soya na sukari

Maandalizi; dakika 15
Muda wa kupika; dakika 30
Muda jumla; dakika 45

Mahitaji

Kwa kuku

1kg vipapatio vya kuku
Chumvi kwa kuonja
Vijiko 6 vya chakula potato starch au corn starch
Mafuta ya kukaangia

Kwa sosi

Vijiko 2 vya chakula mafuta ya kupikia
Kijiko cha chakula kitunguu saumu na tangawizi
3/4 kijiko cha chai pilipili ya kukausha (chilli pepper flakes)
1/3 kikombe sosi ya soya
1/4 kikombe rice syrup au corn syrup
Kijiko 1 cha chakula sukari ya brown
Kijiko 1 cha chai mbegu za ufuta

Maelekezo

Hatua ya 1; andaa kuku na viungo

Osha na kukausha vipapatio vya kuku, kisha kata nusunusu, visiwe vizima. Vipake chumvi

Weka potato starch/ corn starch kwenye sahani pana. Paka kuku kipande kimojakimoja mpaka afunikwe kabisa

Hatua ya 2; kaanga kuku

Chemsha mafuta kwenye kikaangio katika moto wa juu kiasi. Mafuta yakichemka vizuri, ongeza kuku. Weka kipande kimojakimoja na hakikisha havijazani sana. Kama kikaangio chako ni kidogo, kaanga nusunusu. Kaanga mpaka vipate rangi ya kahawia kwa mbali, dakika 8 mpaka 10. Toa kwenye mafuta, weka kwenye chujio au sahan yenye tissues ili mafuta yachuje. Acha ipumzike kwa dakika kama 5

Chemsha tena mafuta, rusisha kuku kwenye mafuta. Kaanga kwa dakika 6 hadi 8 nyingine, au mpaka kuku awe crispy na apate rangi nzuri ya kahawia. Toa kwenye mafuta

Hatua ya 3; andaa sosi

Kwenye kikaango kikubwa katika moto wa juu kiasi, chemsha mafuta ya kupikia kwa ajili ya sosi. Ongeza kitunguu saumu na tangawizi, pika mpaka vilainike, kama sekunde 30 kisha ongeza sosi ya soya, rice/corn syrup, pilipili ya kukausha na sukari. Pika kwa dakika chache ukigeuza mara kwa mara isiungue mpaka sukari iyeyuke

Hatua ya 4; changanya kuku na sosi

Ongeza kuku kwenye sosi. Ipua kwenye moto, changanya mpaka kuku ashike sosi vizuri

Pakua kama utakavyopenda

Nyunyizia mbegu za ufuta kwa juu. Enjoy

Leave a Reply