Mayai ya kukaanga na siagi na maziwa (scrambled eggs)

Maandalizi; dakika 5
Muda wa kupika; dakika 5
Muda kwa jumla; dakika 10

Mahitaji

Mayai makubwa 2
Vijiko 6 vya chakula maziwa fresh
Kijiko 1 cha chai siagi
Chumvi kwa kuonja

Maelekezo

Piga mayai, maziwa na chumvi kwenye bakuli la wastani, mpaka yachanganyike vizuri

Yeyusha siagi kwenye kikaangio kisichoshika chini (non-stick frying pan) katika moto wa chini kiasi. Ongeza mchanganyiko wa mayai

Acha yachemke kwa sekunde 10-20 bila kugeuza; kisha anza kukoroga

Koroga mpaka yaive kama utakavyopenda

Pakua kama utakavyopenda

Enjoy

Leave a Reply