Pancakes za nazi, iliki na ndizi mbivu

Maandalizi; dakika 10
Muda wa kupika; dakika 20
Muda kwa jumla; dakika 30

Mahitaji

Kikombe 1 unga wa ngano, uliochekechwa
Vijiko 2 vya chai baking powder
Vijiko 3 vya chakula sukari
½ kijiko cha chai iliki ya unga
¼ kijiko cha chai chumvi
Mayai 2
300ml tui la nazi
Ndizi mbivu 1-2
Siagi ya kupaka kwenye kikaango

Maelekezo

Katakata ndizi

Kwenye bakuli kubwa, changanya vizuri viungo vikavu vyote; unga wa ngano uliochekechwa, sukari, chumvi, baking powder na iliki

Ongeza mayai na tui la nazi, koroga mpaka uchanganyike vizuri

Paka kikaangio siagi kidogo sana katika moto wa chini. Ongeza ¼ kikombe mchanganyiko wa unga. Weka vipande kadhaa vya ndizi juu yake. Pika mpaka upande wa chini uwe kahawia, na pancake itune kwa juu

Geuza upande wa pili, pika mpaka pancake iive vizuri; kama dakika 1. Pakua kwenye sahani, rudia kwa unga uliobakia

Pakua kama utakavyopenda na sosi utakayopenda

Enjoy

Leave a Reply