Rosti ya egg chops za nazi

Maandalizi; dakika 5
Muda wa kupika; dakika 20
Muda jumla; dakika 25

Mahitaji

Vijiko 2 vya chakula mafuta ya kupikia
Kitunguu maji 1
Nyanya 2
Pilipili kichaa 2
Kijiko 1 cha chai kitunguu saumu na tangawizi
Kijiti cha mdalasini
Karafuu punje 4
Iliki punje 6
Kijiko 1 cha chakula curry powder
Kijiko 1 cha chakula beef seasoning
1/2 kikombe tui la nazi
1/2 kikombe cooking cream
Chumvi kwa kuonja
Majani ya giligilani/ dania/ kotimiri kiasi
Egg chops 4, kwa recipe ya egg chops bonyeza hapa

Maelekezo

Weka nyanya, kitunguu maji na pilipili kwenye mashine ya kusagia chakula kutengeneza rojo

Kwenye sufuria katika moto wa wastani, chemsha mafuta kisha weka kitunguu  saumu na tangawizi; mdalasini, karafuu na iliki. Kaanga mpaka harufu ya ubichi iishe na vilainike, kama dakika 2

Ongeza rojo ya nyanya-kitunguu-pilipili, beef seasoning na curry powder, . Changanya vizuri halafu funika na mfuniko. Acha mchanganyiko uive katika moto wa chini kwa dakika 6 hadi 8, au mpaka nyanya na viungo viive vizuri kabisa

Ongeza tui la nazi na cooking cream. Ongeza na chumvi ikihitajika. Pika kwa moto wa chini kiasi kwa dakika kama 5. Ongeza majani ya kotimiri/ dania/ giligilani halafu uweke egg chops taratibu, geuza zipate sosi pande zote. Kuwa muangalifu zisibomoke.

Acha mchanganyiko uive kwa dakika kama 2 nyingine

Pakua kama utakavyopenda

Enjoy

Leave a Reply