Icing sugar ya jibini (cream cheese)

Maandalizi; dakika 15
Muda jumla; dakika 15

Mahitaji

¼ kikombe siagi
½ kikombe jibini (cream cheese)
Vikombe 2 icing sugar
Kijiko 1 cha chai vanilla extract
Vijiko 2 vya chakula maziwa, na zaidi ikihitajika

Maelekezo

Katika bakuli kubwa, koroga siagi na jibini (cream cheese) mpaka ilainike vizuri

Ongeza icing sugar na vanilla. Endelea kukoroga kwa dakika 1 hadi 2; halafu weka maziwa kidogokidogo mpaka upate uzito unaohitaji

Tumia kama inavyohitajika kwenye keki kama keki ya vanilla; kwa recipe ya keki bofya hapa

Pamba na kukatakata kama utakavyopenda

Enjoy

2 Replies to “Icing sugar ya jibini (cream cheese)”

Leave a Reply