Keki ya Vanilla

Maandalizi; dakika 20
Muda wa kupika; dakika 50
Muda kwa jumla; Saa 1 dakika 10

Mahitaji

250g siagi (robo kilo)
250g Sukari (robo kilo)
4 Mayai
500g Unga wa ngano (nusu kilo)
1 Kijiko cha chakula baking powder
10 Vijiko vya chakula maziwa fresh
1 Kijiko cha chakula vanilla
1 Kijiko cha chai chumvi

Maelekezo

Washa oven 165 C ipate moto wakati unachanganya keki. Paka siagi na unga wa ngano chombo cha kuokea keki, weka pembeni

Kwenye bakuli la wastani, chekecha unga wa ngano, chumvi na baking powder weka pembeni


Kwenye bakuli kubwa, changanya sukari na siagi mpaka ilainike

Ongeza mayai; moja baada ya jingine pamoja na vanilla. Changanya vizuri

Weka mchanganyiko wa unga wa ngano, koroga hadi uchanganyike vizuri

Malizia kwa kuweka maziwa huku ukikoroga mpaka unga ulainike kabisa

Mimina mchanganyiko wako kwenye chombo cha kuokea ulichapaka mafuta awali

Oka keki kwa dakika 35 hadi 50 kutegemea na chombo cha kuokea; au mpaka iive vizuri. Ikiiva, acha ipoe kiasi kabla ya kuiweka kwenye sahani

Ipua keki kwenye sahani au waya wa kuwekea chakula

Mwagia icing sugar kwa juu ukipenda

Katakata kama utakavyopenda

Enjoy

 

44 Replies to “Keki ya Vanilla”

  1. Pole dear, ni kujaribu tu. itakuwa moto ulikuwa mkali labda ikaivisha nje siyo ndani. Ahsante kwa kujaribu, ukiwa na swali lolote uliza

  1. ukitaka keki ichambuke usichanganye sana ule mchanganyiko wako, changanya kiasi tu, hata unga unga kidogo ukibaki itatoka vizuri, hakikisha mchanganyiko usiwe mlaini sana pia

  1. ndio, unapaka siagi na unga kiasi, ila hiyo haiingiliani na keki kutokuiva katikati, ni kusaidia isishike kwenye chombo ikiiva. Kutokuiva itakuwa ni moto, unatumia mkaa au umeme?

 1. Nimepika leo haijaiva ndani vzr, yan haijachambuka lkn nimefuata vipimo kama ulivyosema..nimetumia oven…nilibake for 35 mints kuicheck nikaona haiachi unga kwenye spoke nikaasume imeiva….duu kuja kuikata haijaiva vzr na haijachambuka ila ntaendelea kujaribu…ahsante sana.

  1. Pole my dear, inategemea na chombo unachookea, kama ni bundt yenye tobo katikati inaiva haraka, kama chombo cha kawaida inahitaji muda zaidi, usikate tamaa next time iache muda mrefu:(

 2. kwa wote, kipimo rahisi cha keki kama hujui vipimo ni: unga 1, mayai, sukari na siagi nusu yake. kwa mfano. unga vikombe vinne basi sukari, siagi na yai ni mbili, yaani sukari vikombe viwili, siagi viwili na mayai mawili

 3. Nilikuwa natumia unga nusu, blueband nusu, sukari robo na mayai saba ila keki ikawa haichambuki. Kumbe vingine ni nusu ya unga

 4. Nimepika kwa kutumia vipimo ulivotoa, yaani it’s just wow! Nimefurahi hatari japo naona kama baking powder ilikua imezidi sijui kijiko changu ni kikubwa but kimetoka kitu kizuri nilichokua na wish kitokee

Leave a Reply