Viazi vitamu vya kuponda

Maandalizi; dakika 5
Muda wa kupika; dakika 25
Muda jumla; dakika 30

Mahitaji

500g (nusu kilo) viazi vitamu
½ kikombe maziwa
Kijiko 1 cha chakula siagi
Kijiko 1 cha chakula asali au maple syrup
Chumvi kwa kuonja (ukipenda)

Maelekezo

Menya, katakata na kuosha viazi

Kwenye sufuria katika moto wa wastani, chemsha viazi hadi vilainike kabisa

Chuja maji kisha ponda kwa kutumia mashine au kijiko cha kubondea viazi, mpaka vilainike kabisa

Ongeza siagi na maple syrup/ asali kwa kuonja. Ongeza maziwa kidogokidogo ukianza na ¼ mpaka upate uzito utakaopenda.  Ukipenda weka na chumvi kwa kuonja. Rudisha kwenye jiko kwa sekunde chache ukipenda joto zaidi

Tenga cha moto kama utakavyopenda

Enjoy

 

Leave a Reply