Vitumbua vya nazi na iliki

Maandalizi; dakika 15
Muda wa kusubiri; usiku kucha
Muda wa kupika; dakika 30
Muda jumla; dakika 45 na muda wa kusubiri

Mahitaji

Vikombe 2 mchele
Vijiko vya chai 1¼ hamira
Vikombe 1½ tui la nazi
Kijiko cha chai ½ chumvi
Kikombe cha chai ½ sukari
Kijiko 1 cha chai iliki iliyosagwa
Kikombe cha chai ½ mafuta ya kupikia

Maelekezo

Osha na kuloweka mchele usiku kucha. Chuja maji, weka pembeni

Chemsha tui la nazi kwa sekunde 30 au mpaka liwe ya uvuguvugu kiasi katika moto wa wastani

Katika mashine ya kusagia, weka mchele, tui la nazi, iliki, sukari, chumvi na hamira. Saga mpaka ilainike vizuri. Kama mashine yako ni ndogo, weka kidogo kidogo mpaka umalize mchanganyiko wote. Mimina mchanganyiko kwenye bakuli

Funika bakuli, acha mchanganyiko uumuke kwa lisaa 1, au mpaka ujazo uzidi mara mbili yake

Chemsha chuma cha vitumbua katika moto wa wastani. Weka mafuta kwenye kila shimo la chuma cha vitumbua. Mwagia mchanganyiko kwa ujazo robo tatu ya kila shimo. Acha vitumbua vianze kuiva kwa dakika 2 hadi 3, au mpaka vianze kuwa na rangi ya kahawia na kona zianze kukauka kiasi

Kwa kutumia kijiti cha mishikaki, geuza kitumbua upande wa pili. Acha viive kwa dakika nyingine 3, au mpaka viwe na rangi ya kahawia

Ipua vitumbua, weka kwenye bakuli lenye tissues za jikoni ila mafuta yachuje. Vinaweza kuliwa vya moto au vya baridi

Enjoy!

40 Replies to “Vitumbua vya nazi na iliki”

  1. Nitashukuru sana ukinipa feedback, ni kazi rahisi sana kupika. Kuwa tu muangalifu moto usiwe mkali vikababuka nje visiive ndani

 1. Jane mchere gani umetumia wakawaida , VIP , au mchele wazamani ?
  Kwasababu watuwanadai mchele mpya huwa au Fai nikweli??

  1. Nimetumia mchele wa kawaida ila sisi kwetu hakuna mchele mpya, ni vizuri ukitumia wa zamani ila kama una mpya unaweza pia kutumia, tofauti siyo kubwa sana.

 2. Wajameni Jane we mgomvi. Aaaah mpaka natamani ni drive to Berlin. Nitext basi kikaango wapi ninunue ..heee chinekeee. 😍😍😍 thank you so much..let me paste it in the group..

 3. Asante Jane ntajaribu kupima ntakupa feedback. Je unaweza zaga mchele kwa blenda y juice km una ya kusagia Michele nauliza.

 4. Dada Jane ,what if mtu hana hizo aina zote mbili za machine zakusagia mchele either blender or hiyo nyingine. Je atumie nn kingine for kusaga hizo things?

 5. Hiyo kikaangio mbona amazon USA sikioni? Kuna jina lingine? Hii link yako iko ya kijerumani lugha haipandi. I can’t tell how much will it be in us dollars. Pls help
  Your recipe looks like something I can try but hicho kikaangio sasa.

Leave a Reply