Minofu ya kuku ya kitunguu saumu na pilipili

Maandalizi; dakika 10
Muda wa kumarinate; masaa 2
Muda wa kupika; dakika 10
Muda jumla; dakika 20 na muda wa kumarinate

Mahitaji

Gram 400 minofu ya kuku
Kijiko 1½ cha chai kitunguu saumu na tangawizi
Vijiko 2 mafuta kwa ajili ya kumarinate
Vijiko 2 mafuta kwa ajili ya kukaangia
½ kijiko cha chai red chilli flakes
Chumvi na pilipili manga kwa kuonja
Kijiko 1½ cha chai beef seasoning

Maelekezo

Mchanje kuku awe na sehemu za kutosha viungo kuingia

Kwenye bakuli dogo, changanya beef seasoning, vijiko 2 vya chakula mafuta, red chilli flakes, chumvi, pilipili manga, kitunguu saumu na tangawizi

Weka kuku kwenye bakuli kubwa, ongeza mchanganyiko wa viungo. Changanya vizuri kuku akolee viungo.  Funika bakuli, weka kwenye jokofu kwa masaa 2

Weka kuku kwenye kikaangio chenye vijiko 2 vya mafuta yaliyochemka katika moto wa wastani. Acha aive upande mmoja hadi awe na rangi ya kahawia, asiungue; geuza upande wa pili, acha apike hadi aive vizuri, angalia asikauke

Pakua na chakula au salad kama utakavyopenda

Enjoy

 

Leave a Reply